Wanafunzi wanaosoma vitivo vya sayansi na utafiti wametakiwa kutumia utafiti na ubunifu katika kufanya uzalishaji bora wa bidhaa ambazo zitasaidia kutangaza taifa kwenye masoko kimataifa .
Akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya utafiti na ubunifu uliofanyika katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkoani Iringa [MKWAWA ] Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) Prof .Joseph Ndunguru amesema watafiti wanapaswa kufanya kazi yao ili kuzifanya bidhaa kutoka Tanzania kukubalika kimataifa
“Ni lazima utafiti na ubunifu ufanyike ukiwa wewe na kiwanda ambacho kinazalisha bidhaa moja hauwezi kucompet na masoko ya kimataifa ndo maana kwenye viwanda vya wenzetu kila kiwanda utakuta kina unit au kuna idara pale ya utafiti na ubunifu na kazi yao ni kufanya utafiti wa namna ya kuzalisha bidhaa mpya au kuzalishaa bidhaa yenye sifa ili kucompete na soko la kimataifa “ alisema Prof Ndunguru
Katika hatua nyingine Prof. Joseph Ndunguru amvitaka vyuo kuwaanda wataalamu bora watakaokubalika katika soko la ajira huku akiwataka wanafunzi kutumia tafiti zao ili kujenga kesho ya taifa .
“Vyuo vya Elimu ya juu vinatakiwa kuwaandaa wataalamu bora wenye sifa naujuzi unaohitajika kwenye soko la sasa la ajira tunapokwenda kuimarisha ushirikiano wetu na viwanda na tukumbuke maneno ya aliyekuwa rais wa Africa kusini Nelson Mandela kwamba elimu ni silaha yenye nguvu zaidi ambayo unaweza kubadilishia ulimwengu hivyo tutumie elimu na tafiti zetu ili kujenga kesho ya taifa letu ya wahitimu wenye uwezo wa kutumikia viwanda vyetu ili kujnga uchumi wa viwanda kwa taifa letu “alisema
Kwa upande wake Shadrack Edson Mbunifu kutoka chuo kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa ambaye amebuni mkaa unaotengenezwa na maboksi amesema ametengeneza mkaa huo kwani unamsaada kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuikomboa jamii na matumizi ya mkaa wa kuni ambao umekuwa ukipelekea ukame kutokana na ukataji wa miti hovyo.
“Mkaa huu unachukua dakika 25 kuna aina nyingi za mkaa lakini kutengneza ni rahisi ,haiitaji sana gharama maboksi yanapatikana kwa sababu huwa tunatumia kama takataka ,pia ni environmental friend mkaa huu hauna madhara kwa jamii kuna ukataji wa miti hivyo saa nyingine tunapelekea ukame na hata kusababisha mmomonyoko wa udongo “ Alisema