Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi mohamed mchengerwa amewataka Madiwani na wakurugenzi wa halmashauri kuacha malumbano na na migongano kati ya Wakurugenzi ,Madiwani na mamea.
Mchengerwa ameyasema hayo alipohudhuria Mkutano wa 38 wa ALAT alipozungumza kwa niaba ya Rais Samia ambapo wadau mbali mbali ikiwemo Benki ya NMB kwenye mkutano huo uliofanyika Visiwani Zanzibar.
Pia waziri wa Tamisemi ametangaza vigezo vitakavyo tumika kuwapima viongozi hao wa halmashauri na majiji kwa kutengenezwa vyanzo vipya vya mapato ili kuwapima utendaji kazi kwenye mapato ya makusanyo.