Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu leo amezungumza LIVE kupitia ukurasa wake wa Facebook akiwa ughaibuni na kutangaza nia ya kugombea Urais nchini Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa October 2020.
Pamoja na mengine, Tundu amesema “Kama Rais Serikali yangu haitolipiza kisasi vya mabaya mengi ambayo Wananchi wetu, Mimi, Viongozi na Wanachama wenzangu tumefanyiwa na utawala huu na hata Serikali za nyuma, badala ya kulipiza kisasi Serikali yangu itarudisha, kujenga na kuimarisha mapatano na maridhiano ya kitaifa yatakayojengwa katika misingi ya ukweli juu ya makosa yaliyofanyika, msamaha kwa watakaotubu makosa yao na fidia kwa Wahanga wa makosa hayo”
“Nitaendelea kufafanua haya na mengi mengine katika siku, wiki na miezi inayofatia na wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu endapo nitapata ridhaa ya Chama changu ya kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano, naamini ninazo sifa zote stahiki za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu”
“Kwa zaidi ya miaka 20 nimetetea haki na maslahi ya Wananchi wa Tanzania katika maeneo mbalimbali ya Nchi yetu, nilikuwa wa kwanza kupiga kelele ukandamizaji mkubwa na dhuluma waliyokua wanafanyiwa Wananchi kwenye maeneo mbalimbali ya Nchi yenye utajiri wa madini, kwa miaka 7 kabla ya risasi 16 za Watu wasiojulikana wa utawala wa Magufuli hazijaniondoa Bungeni na Tanzania, niliongoza mapambano ya haki, utawala wa sheria na haki.. niliongoza na kuratibu harakati za kupigania katiba mpya Bungeni’
“Nimekua Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika kabla ya Uongozi wangu kukatishwa kikatili na waitwao Watu wasiojulikana September 7 2017, msimamo wangu katika maswala yote muhimu ya Nchi yetu na ya Watu wetu unajulikana wazi na wote na haujawahi kutetereka” tazama video nzima ya Lissu akiongea kwa kubonyeza >>> HAPA <<<
.