Kama ulikuwa umepitwa na show ya Mkasi, ilikuwa ni zamu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu (Chadema), mengi kayazungumza humu ikiwemo kuhusu Uchaguzi, Sakata la Escrow na katiba mpya.
Ishu ya sakata la Escrow; “Escrow ni moja ya mlolongo mrefu wa matumizi mabaya ya madaraka na ndio maana hii escrow kuna majaji wapo kwenye mgawo wa haya mabilioni ya Escrow kuna mmoja tunaambia amepelekewa milioni 500 hajatajwa kati ya wale waliotwaja lakini tumefuatilia, kuna jaji tena mahakama ya rufani kapelekewa milioni 500…..’
Mtu anayeweza kupokea rushwa namna hiyo wewe usiyeweza kumlipa ukiwa na kesi yule asiyeweza kumlipa unapata haki, kamati ya Zitto imesema na wameleta ushahidi ili gavana wa Bank Kuu Beno Ndulu aruhusu pesa hizo zitoke alipata barua kutoka kwa afisa mmoja wa ikulu ya rais bw. Prosper Mbena kwa hiyo ni system ambayo haiwajibiki kwa mtu yoyote kwa hiyo jibu la swali tulikosea wapi kwa maoni yangu tulianza kukosea mwaka 1962…“ hapa alikuwa akizungumzia ishu ya Escrow.
Kwa maoni yangu mimi imetufundisha tuache visingizo hata sisi tuna visingizo vitu sana wezi wezi wezi sisemi hakuna wezi lakini wizi uwa unawezeshwa ukiacha mlango wazi usiku vibaka wakaingia wakakuchapa yes vibaka wezi lakini kwanini uliacha mlango wako wazi tukifanya kazi kwenye chaguzi tukafundisha wagombea wetu, makala wetu vitu vya kufanya tunafanya vizuri haijawahi kutokea watu wameaguliwa wasigombea kama ilivyotokea kwenye uchaguzi huu wa mwezi uliopita, wilaya ya kilindi mkoa wa Tanga wagombea wetu wote waliondolewa, wilaya ya korogwe vijijini 94 wagombea wetu waliondoka kwa visigizio kwamba mmejaza fomu vibaya ni uhuni...’ hapa akizungumzia chaguzi zilizofanyika.
Ni katiba ya CCM kwasababu imepitishwa na wana CCM tuliona wanavyotaka kututumia kupitisha katiba ya CCM halafu waje waseme na Ukawa walikuwepo na ndio maana tuliondoka kwa hiyo waliobaki kujadili katiba mpya ni CCM na la pili angalia maudhui yake inaangalia inasema nini na haisemi nini, ina yale yale ambayo CCM wameyasema...’ hapa akizungumzia kuhusu katiba.
‘Kwasababu Kuna watu wanapenda ieleweke hivyo kuna watu wanalipa fedha nyingi sana ili hiki chama kionekana chama cha Wachaga na kama kikionekana ni chama chama cha wachaga maana yake kwamba sisi tusiokuwa wachaga sio chama chetu hatutaenda huko, hizi ni siasa unaweza ukaziita ni siasa za maji taka lakini ni siasa ni sehemu za mapambo ya kisiasa…‘ hapa akizungumzia kwanini chama cha Chadema kinaitwa chama cha Wachaga.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter ,Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook