Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky ametoa wito hii leo wa kupata suluhu ya dharura kuhusu mvutano ulioibuka ya ombi la Poland la kuipelekea Ukraine ndege za kivita wazo ambalo Ujerumani, Canada na Marekani wamelipinga.
Jana Marekani nayo ilipingana na Poland kuhusu wazo la kupeleka ndege hizo aina ya MiG-29 za enzi ya kisovieti nchini Ukraine kupitia kambi ya jeshi la anga la Marekani iliyopo Ramstein Ujerumani, hata hivyo Marekani na Nchi nyingine za Ulaya waliipelekea Ukraine silaha ikiwa ni pamoja na vifaru lakini hawakupeleka ndege za kivita kwa wasiwasi wa kuchochea ugomvi zaidi na Urusi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa Berlin na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau wameonyesha kutokukubaliana na Poland kwenye wazo la kupeleka ndege hizo Nchini Ukraine wakisema wanataka vita hii imalizike na sio kuichochea.