Jeshi la Israel lilisema Ijumaa kuwa wanajeshi 117 wamekufa huko Gaza tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini.
“Tunafanya kazi pamoja na vyombo vya usalama, na kwa njia zote za kijasusi na kiutendaji ili kuwarudisha mateka wote nyumbani,” jeshi lilisema.
Marekani, ambayo inatoa msaada wa kijeshi wa mabilioni ya dola kwa Israel, imeunga mkono kwa nguvu jibu lake kwa mashambulizi ya Hamas, lakini imeelezea wasiwasi wake juu ya vifo vya raia na mpango wa muda mrefu wa Gaza.
“Hatuamini kwamba ni jambo la maana kwa Israel, au ni sawa kwa Israel,…kuikalia tena Gaza kwa muda mrefu,” Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan alisema Ijumaa baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Yoav. Gallant huko Tel Aviv.
Gallant alionya kwamba mapambano ya Israel na Hamas “yatahitaji muda — yatadumu zaidi ya miezi kadhaa, lakini tutashinda na tutawaangamiza”.