Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliapa Alhamisi kujibu juhudi za kuwadhuru Waisraeli, wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa jibu linalowezekana la Irani kwa madai ya Israeli kumuua kamanda mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Syria.
Akizungumza katika mkutano wa baraza la mawaziri la usalama mara baada ya mazungumzo yake ya simu na Rais wa Marekani Joe Biden, Netanyahu alisema “Iran imekuwa ikitenda dhidi yetu kwa miaka mingi – moja kwa moja na kupitia washirika.
Na, kwa hivyo, Israeli inachukua hatua dhidi ya Iran na washirika wake – kwa kujihami na kukera.”
Netanyahu aliongeza: “Tutajua jinsi ya kujilinda, na tutatenda kulingana na kanuni rahisi: kwamba wale wanaotudhuru au wanaopanga kutudhuru, tutawadhuru.”