Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania TFF leo Alhamisi ya August 31 2017 imetangaza kumuandikia barua ya onyo kali winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva kwa kosa la kumsukuma muamuzi wakati akiwa Yanga.
Msuva ambaye alikuwa anatuhumiwa kufanya kosa hilo akiwa pamoja na wenzake Deus Kaseke na Obrey Chirwa, yeye pekee ndio amekutwa na hatia wakati Kaseke na Chirwa hajakutwa na hatia ya kutenda kosa hilo, AyoTV ilitembelea mazoezi ya Taifa Stars na kuzungumza na Msuva.
“Kwa upande wangu kwanza naweza kusema kwenye mpira kuna kile kitu kwamba damu ikishachemka lakini sio kwamba nilidhamiria lakini maamuzi waliyotoa ya onyo nimeyapokea lakini nimeomba radhi kwa kilichotokea”>>> Msuva
Maswali sita aliyoyajibu Msuva baada ya kuwasili Airport DSM akitokea Morocco