Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori ni hii ya kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Watanzania milioni 39 wanakunywa mataputapu’
#JamboLEO Utafiti WHO umeonesha 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, Dar, K'njaro zaongoza kwa wanywaji pic.twitter.com/OtebZRHH9i
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
Gazeti hilo limechapisha utafiti uliofanywa na shirika la Afya Dunia ‘WHO’ umeonesha kuwa 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, huku mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro ikiiongoza kwa kuwa na wanywaji wengi wa pombe hiyo.
Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.
Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.
Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene. Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawwake ‘TAMWA’.
#NIPASHE CHADEMA kanda ya pwani yapiga marufuku mameya kuhudhuria mikutano wadai mameya wao wamekuwa wakidhalilishwa pic.twitter.com/rLueZKlCsc
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#NIPASHE Polisi wasema kuna utata kifo cha Profesa UDSM ambaye alidaiwa kujipiga risasi kwa bahati mbaya pic.twitter.com/JEBFYTYAnm
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#NIPASHE Uongozi CCM umewaonya wabunge wake wasiohudhuria vikao vya Bunge huku baadhi yao wakitakiwa kujieleza pic.twitter.com/fdXYU3wHA6
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#MWANANCHI Meli ya mizigo yazama Z'bar, baadhi ya wananchi watumia fursa hiyo kujichukulia bidhaa zilizokuwamo pic.twitter.com/LucWcxaJ9p
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#MWANANCHI Serikali imeendelea kutangaza mpango wa kufufua kiwanda cha General Tyre kwa kununua mashine mpya pic.twitter.com/Zf6Wk7Iiuy
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#MWANANCHI Adaiwa kuiba mtoto mchanga Tarime ili kumdanganya mumewe kuwa amejifungua kwa lengo la kuinusuru ndoa pic.twitter.com/mqgFsRLUHX
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#MWANANCHI Mawakili 'kanjanja' wanaswa kortini Moshi, wadaiwa kuingia mahakamani na kujitambulisha kuwa ni mawakili pic.twitter.com/5wAKaUBfE0
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#MWANANCHI Zaidi ya watu mil 2.1 Uingereza wasaini waraka wa mtandaoni wataka kura ya pili ya maoni kujitoa EU pic.twitter.com/kej4ZKrNeQ
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#MWANANCHI Serikali ya Sudan Kusini imesema haitasherehekea uhuru wake mwaka huu kutokana na ukata wa fedha pic.twitter.com/kvAEXsaQFU
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#HabariLEO Rais Magufuli ateua ma-DC 139, ma-RC watatu, sura ngeni zatawala, wazee wengi waenguliwa pic.twitter.com/rBic5imgLi
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#HabariLEO Wachumi waonya benki utozaji wa 18% ya VAT, wasema benki zinao uwezo kuepusha mzigo huo kuangukia walaji pic.twitter.com/FCHfEs0ZoN
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#HabariLEO Serikali imetoa mwito kwa watumishi wake kuacha kuchagua maeneo ya kufanya kazi na kuwa wazalendo pic.twitter.com/0DW8OqMnDm
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
#RaiaTANZANIA TRA: mfumo wa miaka iliyopita wa Serikali kufanya kila kitu unasababisha ugumu katika ukusanya kodi pic.twitter.com/ab0EYrn2gC
— millardayo (@millardayo) June 27, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 27 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE