Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimekuwekea hapa kubwa za leo kutoka kwenye magazeti ya Tanzania, waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
#NIPASHE Ripoti iliyotolewa na Waziri Mhagama inasema maambukizi mapya ya VVU yamepungua kwa wastani wa 0.4% kulinganisha na mwaka uliopita pic.twitter.com/MWWDEHCTzo
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Mabasi yaendayo mikoani kituo cha mabasi ubungo yakosa abiria, inadaiwa basi la abiria 60, linaweza kuondoka likiwa na wasafiri 10 pic.twitter.com/ACMKdyj1EL
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE DPP awafutia kesi ya uhalifu wa mtandao wafuasi watano CHADEMA na wenzao watatu baada ya kuona hana nia ya kuendelea na mashtaka pic.twitter.com/Q6XVY5xnHA
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Baba kortini Kigoma kwa kutuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kufariki dunia pic.twitter.com/B0EGVbnQiV
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Idadi ya wanaoshtakiwa kwa mauaji ya watafiti ktk kijiji cha Iringa Mvumi Dodoma imeongezeka na kufikia 29 baada ya 12 kuunganishwa pic.twitter.com/t4t6vZ494h
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Mkazi wa kitongoji cha Mugaza, Bukoba Renatus Gamanywa ametiwa Mbaroni kwa tuhuma za kumuua dada yake na kumzika shambani kwao pic.twitter.com/nd58eCNA97
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, amelazwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, 'JKCI' baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake pic.twitter.com/x62kYHW45l
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Askari wa JWTZ anashikiliwa na polisi Arusha baada ya kukutwa akiwa na wahamiaji haramu nane kutoka Ethiopia pic.twitter.com/kWIKleV50y
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE TAKUKURU Kigoma yachunguza idara ya afya kuhusu matumizi ya mil 900 zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya shughuli za idara hiyo pic.twitter.com/hnKK6tvH53
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Ndege iliyoanguka Colombia wakati inaanguka hakukua na mlipuko, wataalamu wanasema ni dalili za ndege kuwa haikuwa na mafuta pic.twitter.com/yHDEK0tg05
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Hospitali ya MUHAS Mloganzila kuanza kutoa huduma zake February mwakani pamoja na kufundisha wanafunzi wa masomo ya vitendo pic.twitter.com/84ZdlfD9AT
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#NIPASHE Ngassa ashangazwa na habari za yeye kusaini Mbeya City, asema alikutana na ofisa habari wa timu hiyo kwa mazungumzo ya kawaida pic.twitter.com/5L0cGxuY76
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Biashara ya usafiri wa anga nchini yazidi kuporomoka, ikiathiri kampuni, ajira na kipato cha huduma zinazoambatana na usafiri huo pic.twitter.com/MUKvHzt4Gj
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Wafanyabiashara kutoka Vietnam washindwa kusafirisha Korosho tani 3,800 kutokana na ukosefu wa meli na kuzuiwa kutumia barabara pic.twitter.com/9CdafpNiHt
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Utafiti uliofanywa na Twaweza umebaini 92% ya wananchi wanataka 'Bunge live' huku 79% wamepinga uamuzi wa Serikali kuzuia pic.twitter.com/1NfWorSgsj
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Kituo cha taaluma ya uhasibu DSM kimebainika kujengwa kwa Sh bil 33 badala ya bil 14 kama ilivyopangwa katika bajeti pic.twitter.com/BRx01JSaRo
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI RC Mtwara, Halima Dendego awashusha vyeo walimu 63, asema udanganyifu uliokuwa unafanyika ni wa kuwaharibu watoto kielimu pic.twitter.com/zreg6gDurQ
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Serikali imetenga bil 48 za ujenzi wa mahakama 40 nchini mwaka wa fedha 2016/17 ili kurahisisha utendaji kazi wa watumishi pic.twitter.com/LpfsolBnQF
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Serikali ipo mbioni kujenga mtambo utakaokusanya na kusafisha majitaka kwa ajili ya matumizi mengine pic.twitter.com/Vq3KvkHf9r
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Takwimu mpya zinaonyesha ktk miaka 20 ugonjwa wa saratani ya kinywa umeongezeka kwa asilimia 68 pic.twitter.com/jX4MHUAImu
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Kitengo cha taifa cha dawa Ufaransa kimemsimamisha mzalishaji wa moyo bandia baada ya bidhaa zake kutokuwa na matokeo mazuri pic.twitter.com/PJk0V72rA1
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Athari za mtoto kunyonya kidole
1.Midomo kulegea
2.Mpangilio mbaya wa meno, muonekano mbaya wa sura
3.Matatizo ya kuongea vizuri pic.twitter.com/gOh35clZoH
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MWANANCHI Muuguzi wa zahanati ya Buluma wilayani Kahama Shinyanga amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kumpiga mgonjwa pic.twitter.com/JEg8Uf26dl
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa bei ya saruji imepanda zikiwa ni siku chache baada ya kiwanda cha saruji cha Dangote Mtwara kusimamisha uzalishaji pic.twitter.com/9srWrs7ubV
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MTANZANIA Zaidi ya wanafunzi 200 chuo cha uuguzi Sengerema wagoma kula, kuingia madarasani, wodini wakidai kunyanyaswa na baadhi ya walimu pic.twitter.com/oV4A16a61U
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#TanzaniaDAIMA Tundu Lissu amesema vyama vya upinzani lazima vibadilike ili kukabiliana na Rais Dk. John Magufuli pic.twitter.com/gMBNy9SCNv
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
#MAJIRA Utafiti wa viashiria vya VVU mwaka 2011/12 Tanzania Bara unaonesha idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa VVU kuliko wanaume pic.twitter.com/90gbt8btBo
— millardayo (@millardayo) December 2, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV LEO DECEMBER 2 2016? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA