Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti Septemba 2, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Askofu IKONGO ampongeza SLAA kwa kuwa mkweli na kuwataka Maaskofu wenzake wanaomshambulia wamuache ajibiwe na viongozi wenzake #HabariLEO
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Uwaziri wamtesa RIDHIWANI, apania kurejea Bungeni huku akitamani Uwaziri, Ni endapo MAGUFULI atachaguliwa kuwa Rais #MAWIOGAZETI #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Viongozi watatu wa CCM wadaiwa kumshawishi Dr.SLAA kuondoka UKAWA, viongozi wake wabaini na kuahidi kuweka hadharani #MAWIOGAZETI #SEPTEMBA3 — millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
MBATIA asema madai ya Dr.SLAA kwa LOWASSA yanazidi kuwaongezea kasi ya kwenda Ikulu na kamwe hayawezi kuwarudisha nyuma #MAJIRA #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
MAGUFULI amesema kuna watu wachache wanaipaka matope ya uchafu Serikali wanapotumwa kufanya kazi hivyo atapambana nao #MAJIRA #SEPTEMBA3 — millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
ROSTAM AZIZ ameshangazwa na kauli ya Dr.SLAA na kusema kama alimtishia maisha alishindwa nini kuripoti Polisi #MAJIRA #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Wasimamizi wa nne wa BVR Kahama wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukiuka maadili na taratibu zilizowekwa na NEC #MAJIRA #SEPTEMBA3 — millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Utafiti wa TWAWEZA umeonesha kuwa wananchi watachagua mgombea Urais ambaye atazungumzia sera nzuri ambazo zinalenga kutatua kero zao #MAJIRA
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Serikali imesema itafuatilia suala zima la uagizaji wa dawa feki za mifugo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria #MAJIRA — millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Chopa nne kutumika kumnadi LOWASSA kwa kuzunguka nchi nzima ili kuhakikisha mgombea wao anashinda uchaguzi Mkuu #TzDAIMA #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Taharuki imetokea kwa wakazi wa Dar baada ya pantoni waliyokuwa wamepanda kukosa mwelekeo na kujikita kwenye jiwe #TzDAIMA #SEPTEMBA3 — millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
MBOWE amesema kilichofanywa na Dr. SLAA ni sawa na msafiri kutokea Dirishani wakati treni ikiendelea na safari zake #RaiaTZ #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
MKAPA amesema uaminifu wa MAGUFULI kiutendaji ndiyo nyenzo pekee itakayoliinua Taifa la Tanzania Kimaendeleo #UHURU #SEPTEMBA3 — millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
MWIGULU amewaonya viongozi wa upinzani kuacha tabia ya kutumia hotuba ya Nyerere vibaya kwa kujinufaisha wenyewe #UHURU#SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Dr.SLAA apata wakati mgumu baada ya watu kujitokeza hadharani kumshambulia na kuhoji sababu ya kutoa shutuma hizo kwa LOWASSA #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Masheikh 6 wa Tanzania waliotekwa nyara tangu Agosti13 DRC wameachiwa huru na Serikali inafanya mpango wa kuwarejesha #MWANANCHI SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
JK amesema ili kuwaweka wananchi salama kamera maalum za CCTV zitafungwa katika miji mikuu kukabiliana na uhalifu nchini #MWANANCHI SEPTEMBA
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Watu 90 wamelazwa katika kambi za kipindupindu Dar baada ya kuambukizwa ugonjwa huo,idadi ya waliougua imefikia 635, waliokufa 10 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Mikoa ya kanda ya Ziwa imetajwa kuongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti #MWANANCHI SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Mtoto auawa kwa mganga wa kienyeji Geita wakati akitibiwa ugonjwa wa kifafa, alichomwa kisu kifuani na mtu mwenye tatizo la akili #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Zaidi ya walimu 40 wa Sekondari Kahama wamekesha kwa siku nne mfululizo kwenye ofisi za Manispaa wakidai mishahara yao #MWANANCHI #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA terminal iii unatarajiwa kukamilika 2016 na utagharimu bilioni 518 #MWANANCHI #SEPTEMBA3
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
MBWANA SAMATTA,BOCCO na ULIMWENGU ndiyo wameshikilia mkononi roho za Watanzania ili kuhakikisha wanaipa ushindi Stars Jmosi Taifa #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) September 3, 2015
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos