Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu yaTwitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti November 08, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Rais Dk.MAGUFULI ametangaza kufuta safari zote za nje ya nchi kuanzia jana kwa watendaji wa umma hadi atakapotolea maamuzi mengine #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
MBOWE amesema UKAWA watafanya mkutano kama kawaida licha ya jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya hadhara #NIPASHE #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Baadhi ya wananchi Z’bar wamesema ZEC inapaswa kuvunjwa kabla ya marudio ya uchaguzi kwa kuwa hawana imani nayo tena #NIPASHE #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
TANESCO wamesema kutokana na kukithiri wizi wa umeme kwa baadhi ya watu wasio waaminifu wamelazimika kufanya operesheni usiku #NIPASHE NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Zaidi ya nyumba 80 zimezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo inayoendelea kunyesha Ruvuma #NIPASHE #NOV08 https://t.co/A7tOFS4Zzt
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Wananchi wa Igunga wamegoma kukabidhiwa majengo ya maabara yaliyojengwa chini ya kiwango katika shule za sekondari #NIPASHE #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Yanga imesema inahitaji bilioni 1.3 ili kumwachia mshambuliaji wao wa kimataifa Donald Ngoma kwa timu yoyote inayomtaka #NIPASHE #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Baraza kuu la CUF limekutana na kusisitiza kuwa hawatarudia uchaguzi wa Z’bar, waitaka ZEC itangaze matokeo ya Oktoba 25 #MWANANCHI #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Wabunge 47 viti maalum CCM na UKAWA watoswa, waingiza sura mpya 79, 33 wapitishwa tena kuingia bungeni#MWANANCHI NOV https://t.co/A7tOFS4Zzt
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Arusha imetajwa ni kati ya Mikoa inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaomiliki bastola #MWANANCHI #NOV08 https://t.co/A7tOFS4Zzt
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Kauli ya ‘Hapa kazi tu’ imeanza kuwahamasisha wananchi ambao wameishauri Serikali ifungue ofisi zake siku ya J’mosi hadi saa 7 #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Wakazi wa Arusha wamepitisha sheria ndogo ya kuwachapa viboko 6 hadharani familia zitakazokutwa zinaishi katika mazingira machafu #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Takwimu za sensa ya makazi ya watu mwaka 2012 inaonyesha kuna vifo 432 kwa vizazi hai 100,000 kutoka 454 mwaka 2010 #MWANANCHI #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Watu wanne ndugu wamepandishwa kizimbani Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Katibu wa CCM Mvomero amenusurika kipigo kutoka kwa wanachama wa chama hicho waliokuwa wakilalamika kukatwa mshindi kura za maoni #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Polisi Tanga imewakamata wahamiaji haramu 45 wenye asili ya kiarabu wakiwa ndani ya fuso wakielekea Dar es salaam #MWANANCHI #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Serikali ya Urusi imesitisha safari zake zote za ndege kuelekea Misri huku Marekani ikiimarisha usalama katika ndege zote #MWANANCHI #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Kocha wa Man U amewataka mashabiki wao wamzomee yeye na si wachezaji wake ambao wamelalamikiwa kushindwa kushambulia #MWANANCHI #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Messi ameingia ktk kinyang’anyiro kuwania tuzo ya bao bora mwaka 2015 kutokana na bao alilolifunga kwenye mchezo dhidi ya Athletic#MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Muhimbili bado hawajaanza kutoa vipimo vinavyotumia mashine za CT Scan na MRI kutokana na kuharibika tangu August mwaka huu #MTANZANIA NOV08

Rais Dk.MAGUFULI ameagiza wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari za Serikali waanze kusoma bure kuanzia Januari 2016 #MTANZANIA #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Muhubiri TB Joshua ametuma ujumbe mzito kwa aliyekuwa mgombea Urais LOWASSA uliosema kilichomtokea kinamuandaa kwa mambo mengine #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Rais Dk.MAGUFULI anatarajia kulihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza Nov.20 mwaka huu #MTANZANIA #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Mtoto wa miaka mitano amefariki kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao baada ya mvua kubwa kunyesha Mwanza #MTANZANIA #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Kocha Mourinho amesema kutokana na matatizo yanayompata atashindwa kurudi katika ubora wake kama alivyokuwa mwanzo #MTANZANIA #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Mbwana Samatta leo atakuwa anasaka rekodi ya ufungaji bora Afrika wakati timu yake ya TP Mazembe ikicheza ligi ya mabingwa #MTANZANIA NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Chama cha walimu Dar kimemwomba Dk.MAGUFULI kutatua matatizo yanayowakabili ambayo hayakutatuliwa na rais mstaafu JK #TzDAIMA #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Timu ya Taifa ya wanawake imemuaga nguli Esther Chabruma ambaye ametangaza kustaafu kuichezea timu hiyo #TzDAIMA NOV https://t.co/A7tOFS4Zzt
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
70% ya maji yanayotumiwa na wakazi wa Dar yamechanganyikana na kinyesi cha binadamu huku 30% tu ndiyo safi na salama #MZALENDO #NOVEMBER08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Klabu ya Azam imewakaribisha Yanga wakae mezani kama wanataka kuchukua baadhi ya wachezaji wao katika usajili wa dirisha dogo #MZALENDO NOV8
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Serikali imesitisha matumizi ya picha ya Rais Dk. MAGUFULI katika ofisi za umma na wananchi mpaka hapo itakapotangazwa tena #HabariLEO NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Wakazi wa Mwanza wamempongeza Rais Dk.MAGUFULI kwa namna alivyoanza kazi kwa kufanya ziara ya kushtukiza Wizara ya fedha #HabariLEO #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Siku 3 baada ya Dk.MAGUFULI kuapishwa mwanachama wa CCM ameibuka na kumtabiria mtoto wake wa miaka miwili atakuwa rais 2050 #HabariLEO NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Mbunge mteule wa Butiama NIMRODI MKONO wa CCM ndiye mwenye umri mkubwa zaidi kati ya wabunge wote waliotangazwa na NEC #MTANZANIA #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
#Tweet 2 Ana umri wa miaka 72 akifuatiwa na Margaret Sitta mwenye miaka 69, Mbunge mdogo zaidi ni Holle Vuma wa jimbo la Kasulu ana miaka 25
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Rais Dk.MAGUFULI ametoa agizo katika usimamizi wa manunuzi ya Serikali ambayo yamekuwa yakitumika vibaya kwa kuiibia Serikali #HabariLEO NOV
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Jeshi la Polisi Mbeya linawashikilia raia wanne wa China kwa kosa la kukutwa na pembe 11 zinazodhaniwa kuwa za faru #HabariLEO #NOV08
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Rais wa TFF amesema anafikiria namna ya kumshawishi nyota wa timu ya Taifa ya wanawake Esther Chabruma kujiunga na kozi za ukocha #HabariLEO
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Baada ya mazungumzo yaliyochukua zaidi ya saa mbili kati ya TB Joshua na viongozi wa UKAWA, nabii huyo ameahidi kurudi tena TZ #NYAKATI NOV8
— millard ayo (@millardayo) November 8, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.