Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti November 26, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Uhaba wa fedha za kuendeshea Serikali TZ umetajwa kumtesa Rais MAGUFULI, aamua kusaka njia mbadala ya kukusanya fedha #GazetiRAI #NOVEMBER26
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Rais MAGUFULI ameanza Urais na Serikali hoi isiyo na fedha za matumizi na inayodaiwa huku na kule #GazetiMAWIO >>https://t.co/ELYAj0CuSp — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Serikali imesema imejipanga kuondoa gharama vikao vya kazi vinavyowahusu watendaji kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano ya TEHAMA #RaiaTZ
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Jukwaa huru la Wazalendo limemshauri Rais MAGUFULI kufuta posho za vikao vya Bungeni #GazetiRaiaTZ #NOVEMBER26 >>https://t.co/ELYAj0CuSp — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Binti wa darasa la nne afanya Mtihani wa taifa akiwa chini ya ulinzi, aliachishwa masomo na wazazi wake ili aolewe Mpanda #RaiaTZ NOVEMBER26
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
DC Paul MAKONDA awatia mbaroni kwa saa sita maofisa 20 waliochelewa ziara yake kwa saa tatu #MWANANCHI #NOV26 >>>https://t.co/ELYAj0CuSp — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mahakama Kuu Mwanza kumaliza leo utata wa kesi ya mazishi ya Marehemu MAWAZO, aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA Geita #MWANANCHI #NOV26
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Gavana mmoja Kenya aingia matatani kwa kutumia Mil. 400 za Serikali kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais MAGUFULI #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Siku moja baada ya kufuta Sherehe za Uhuru, Rais MAGUFULI atangaza kufuta maadhimisho ya siku ya UKIMWI #MWANANCHI >>https://t.co/ELYAj0CuSp
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
#TWEET2: Rais MAGUFULI aagiza fedha za maadhimisho ya siku ya UKIMWI zitumike kununulia dawa za ARV #MWANANCHI >>>https://t.co/ELYAj0CuSp — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mradi wa mabasi ya mwendokasi Dar utaanza rasmi Januari 2016, Ofisi ya Waziri Mkuu wafanya mazungumzo na wanaosimamia mradi #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Serikali imetangaza mpango wa kuwaruhusu wanafunzi wa kike wanaopata mimba kuendelea na masomo ili kukabiliana na ukatili #MTANZANIA #NOV26 — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewasili Kenya jana jioni huku akitoa baraka kwa lugha ya Kiswahili #MTANZANIA #NOV26
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mahakama ya Kisutu imeanza kusikiliza maelezo ya mwanafunzi anayetuhumiwa kueneza taarifa za kulishwa sumu Jenerali MWAMUNYANGE #MTANZANIA — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Wananchi Shinyanga wamemkamata muuguzi wa kituo cha afya Kambarage akiwa na dawa za Serikali alizokuwa akipeleka kusikojulikana #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mchakato Mahakama ya kuwashughulikia mafisadi waanza, Jaji Kiongozi amesema hiyo ni sehemu ya utekelezaji ahadi za Rais MAGUFULI #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Serikali imesema haitowavumilia watumishi wa viwanja vya ndege wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na nyara za Serikali #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Njaa yavikumba vijiji 35 Iringa, wananchi wakabiliwa na upungufu wa chakula, walazimika kushindia mlo mmoja,matunda na mboga pori #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Watu 14 wanusurika kuteketea kwa moto Morogoro, nyumba zao zachomwa moto usiku wa kuamkia juzi #GazetiMWANANCHI >>https://t.co/ELYAj0CuSp
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Nyumba 6 Ulanga, Morogoro zimeteketea kwa moto baada ya kuchomwa na watu wasiojulikana, chanzo kikidaiwa ni tofauti za kisiasa #JamboLEO — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mkuu wa Wilaya Babati aagiza Mtendaji wa Kata na Mwenyekiti wakamatwe kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka #MWANANCHI #NOV26
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Jeshi la Polisi Tanga limewakamata wahamiaji haramu 34 raia wa Ethiopia waliokuwa wakiingia nchini bila vibali #MTANZANIA #NOV26 — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Kundi la nyuki limekuwa likiishi ofisini kwa Mwalimu Mkuu shule ya msingi Mapinduzi iliyopo Geita kwa miaka mitatu #MWANANCHI #NOVEMBER26
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Wananchi wa Kahama wameiomba Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha inaharakisha bomoabomoa kwa wananchi waliovamia maeneo ya wazi #MTANZANIA NOV — millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mtu mmoja amefariki akiopoa simu kisimani Tabora, aliazima simu aitumie kisha ikatumbukia, akalazimika kuifuata lakini hakurejea #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Shirika la wanawake Afrika, limeitaka Serikali kufuta adhabu ya viboko mashuleni kwani inachangia ukatili kijinsia na kisaikolojia #JamboLEO
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Sekou-Toure Mwanza amesema Kanda ya Ziwa inaongoza watoto kuzaliwa na ugonjwa wa mdomo wa sungura #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Mgombea Ubunge Arusha mjini Godbless Lema ameanza staili mpya ya kuomba kura kwa kutembea kwa miguu na kuonana na mtu mmoja mmoja #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na KAFULILA itaanza kusikilizwa leo na jaji ambaye alitoa hukumu tata iliyohusisha Escrow #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Muuguzi kituo cha afya Kambarage Shinyanga anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba dawa za Serikali #GazetiUHURU>https://t.co/ELYAj0CuSp
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Tafiti zinaonyesha nchini Uingereza watoto wanaozaliwa mwishoni mwa wiki wanahatari kubwa ya kufariki kuliko wale wa siku za juma @JamboLEO
— millard ayo (@millardayo) November 26, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE