Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti Desemba 13, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
CAG amewaondoa kwenye nafasi za uongozi maofisa wake waandamizi watatu ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za uzembe kazini #MTANZANIA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
MNYIKA amesema Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Rais MAGUFULI limedhihirisha ubovu wa CCM kwa kurudisha watuhumiwa wa Escrow #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu TZ limeandaa mdahalo kujadili hotuba ya Rais MAGUFULI aliyoitoa wakati akizindua Bunge #MTANZANIA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Rais mstaafu MWINYI ameishauri Serikali kupunguza pengo la uhaba wa madaktari na wauguzi ili kuokoa afya za Watanzania #MTANZANIA #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Jumuiya ya vijana CUF imeeleza kusikitishwa na uteuzi wa Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Rais kwa kuwa baadhi wana kasoro #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Mawaziri na Manaibu waziri wapya wameanza kufanya kazi mara baada ya kuapishwa kwa kile kinachoonekana kwenda na kasi ya Rais #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
TRA imesema kuwa wafanyabiashara 15 ambao wameshindwa kutii agizo la Rais la kulipa kodi ndani ya siku 7 watakiona cha moto #MTANZANIA DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Nyota wa Man City na Ivory Coast Yaya Toure amefanikiwa kushinda tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2015 #MTANZANIA #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Kutokana na mwenendo mbaya wa timu ya Chelsea, kocha MOURINHO amesema kuna wachezaji ambao wanamuangusha msimu huu #MTANZANIA #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Hali ya kufanyika kwa uchaguzi wa Rais Z’bar imeonekana kuwa finyu kutokana na kutokuwapo maelekezo ya kuitaka ZEC kuanza kuandaa #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Haikuwa jambo la kawaida wakati hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri 30 ikulu jana ilipofanyika kwa dk.60 bila ya kuwepo shamrashamra #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Watoto 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari bingwa toka Marekani na hapa nchini katika hospitali ya Muhimbili #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Takataka zilizokusanywa maeneo mbalimbali jiji la Dar siku ya sherehe za Uhuru hazijaondolewa kutokana na uchache wa vitendea kazi#MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Siku 3 baada ya Rais MAGUFULI kutangaza Baraza jipya la Mawaziri na kuapishwa jana, viongozi wa dini wameridhishwa na uteuzi huo #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Waziri mkuu mstaafu SUMAYE amejiunga rasmi na CHADEMA huku kukiwa na fununu kuwa ndiye atakuwa mrithi wa Dk.SLAA #MWANANCHI #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
TANESCo Wilaya ya Mwanga imepata hasara ya zaidi ya milioni 150 kwa kipindi cha miezi miwili kutokana na uharibifu wa miundombinu #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Vyama vya CCM na CHADEMA vimeendelea kukabana koo maeneo mbalimbali katika kuwania Umeya na Uenyekiti wa Halmashauri #MWANANCHI #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Utafiti wa awali umeonyesha kuwa Wilaya ya Misungwi imekithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Watoto wawili wamefariki kwa kutumbukia kwenye shimo lililojaa maji lililochimbwa na TANESCO kwa ajili ya kusimika nguzo Geita #MWANANCHI

Kasi ya Rais MAGUFULI kutumbua majipu inatarajiwa kuhamia ndani ya CCM mara atakapokabidhiwa rungu la Uenyekiti na JK #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
CHEDEMA kimeahidi kumshughulikia Bungeni Waziri wa nishati na madini MUHONGO kikidai bado hajasafishwa kwenye kashfa ya Escrow #NIPASHE DEC
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Tume ya haki za bibadamu imemtaka Paul MAKONDA kuacha kutumia vibaya nafasi yake kwa kuwaweka ndani watendaji wa Serikali #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amewapa mwezi mmoja watumishi wa umma wawe wamejaza fomu za tamko la mali na madeni yao #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
TRA imeahidi kugawa bure mashine 200,000 za EFDs kwa kuanzia ikiwa ni jitihada zao za kuhakikisha wanaongeza mapato ya Serikali #NIPASHE DEC
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi LUKUVI amewataka watu ambao wamevamia maeneo ya wazi kuondoka kabla ya bomoa bomoa #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Waziri wa nishati na Madini Prof.MUHONGO amewahakikishia Watanzania kwamba umeme utashuka bei na hautakuwa na mgawo #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala bora SIMBACHAWENE amesema hataki kuona mwanafunzi akikaa sakafuni #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Ununuzi wa meli 4 kwa ajili ya kuhudumia wananchi katika ziwa Tanganyika, Nyasa na Victoria umekwama kutokana na kukosa fedha #NIPASHE DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
DAWASA imesaini mkataba wa bilioni 234 kwa ajili ya kujenga mtandao mpya wa mabomba ya maji kwa wakazi wa Dar es salaam #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya imezindua namba za simu za bure ambazo wananchi watakuwa wanapiga muda wote kuuliza huduma #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Mgombea Ubunge Arusha mjini Godbless LEMA amemchongea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuingilia kampeni za uchaguzi jimboni kwake #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Wilaya ya Hai inakabiliwa na upungufu wa zaidi ya walimu 360 wa shule za msingi, mpaka sasa waliopo ni 1,007 tu #NIPASHE #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Mtoto amuua mama yake kwa kumchoma kisu kifuani kwa madai ya kutompa chakula LINDI, pia amjeruhi baba wakati akimuokoa mke wake #NIPASHE DEC
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Naibu Waziri wa afya KIGWANGALA amesema wameanza kutumbua majipu madogo ktk Serikali na watakaoshindwa kwenda na kasi wakae pembeni #TzDAIMA

Watumishi 15 wa idara ya ardhi na mipango miji katika Manispaa ya Bukoba wanashikiliwa na Polisi kwa kugawa hati kinyume cha sheria #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Kijiji cha Mtanange kilichopo Rufiji kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa shule na kusababisha wanafunzi kuhindwa kusoma #TzDAIMA #DEC13
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Makampuni 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao yamejisalimisha TRA lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku 7 #HabariLEO
— millard ayo (@millardayo) December 13, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE