Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti January 6, 2016, unazisoma zote kwa pamoja.
Oparesheni ya kuondoa mifugo iliyovamia kwa kasi bonde la Kilombero Morogoro yaanza #MagazetiJAN6 #JamboLEO >>https://t.co/4lqjagG8X1
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mbunge wa UKAWA azuia bomoabomoa Dar, Mahakama Kuu yaipiga stop Serikali kuendelea na zoezi hilo #MagazetiJAN6 #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mawaziri wa Rais JPM watumbua majipu, wawili wasimamisha kazi vigogo wa chini yao kwa kushindwa kutekeleza majukumu #MagazetiJAN6 #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Watu watano familia moja wafariki kwa kusombwa na maji,mafuriko yawakuta wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao Kigoma #MagazetiJAN6 #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mamlaka ya EWURA yatangaza kushuka kwa bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa ikilinganishwa na 2015 #MTANZANIA >>https://t.co/jE6H58C7iW
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mhandisi wa Mabasi ya mwendokasi ajikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa akitoa ufafanuzi wa nauli #MTANZANIA>>https://t.co/jE6H58C7iW
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Askari msaidizi wa IGP MANGU aliyepata ajali na kufariki akiwa na familia yake #MagazetiJAN6 #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Wahudumu wa vituo vya afya Dodoma walazimika kusaka maji nje ya hospitali kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa #MagazetiJAN6 #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Waziri Mkuu MAJALIWA awaonya madaktari wanaowatoa mimba wanafunzi, waache kabla ya kuchukuliwa hatua #MTANZANIA JAN6>https://t.co/jE6H58C7iW
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Katibu mmoja Baraza la ardhi Dar afikishwa kizimbani kwa tuhuma za kuomba rushwa sh.150,000 #MagazetiJAN6#MTANZANIA>https://t.co/jE6H58C7iW
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mji wa Dodoma jana ulizizima wakati Polisi walipokuwa wakiaga miili 6 ya marehemu ikiwemo wenzao wawili waliokufa maji juzi #MWANANCHI JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mkuu wa Mkoa Dar amewataka wananchi waliovamia na kujigawia maeneo katika shamba la Waziri Mkuu mstaafu SUMAYE waondoke mara moja #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Rais KAGAME akosoa msimamo wa Marekani unaopinga uamuzi wake kugombea Urais kwa mara ya tatu #MagazetiJAN6 #MAJIRA >https://t.co/4lqjagG8X1
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Baraza la ushauri la watumiaji usafiri wa majini na nchi kavu limepinga nauli za mabasi yaendayo kasi zilizopendekezwa na UDA #MWANANCHI JAN
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Waziri Mkuu amewaonya madaktari vinara wa hospitali ya Rufaa Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
CCM Arusha leo wanaanza kutoa fomu kwa watakaowania nafasi ya M’kiti na katibu wa Itikadi kutokana na waliokuwepo kuhamia CHADEMA #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Watu 1,500 wakumbwa na mafuriko Morogoro na kusababisha hasara ya vitu, wahifadhiwa katika majengo ya mahakama na shule #MWANANCHI #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Manispaa ya Ilala imesema wadaiwa sugu wa kodi ya majengo watakaoshindwa kulipa ankara zao kabla ya April watachukuliwa hatua #MWANANCHI JAN
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Waziri LUKUVI amesema Serikali ya awamu hii imejipanga kuhakikisha ardhi yote inapimwa ili kila Mtanzania mwenye eneo apate hati #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Jiji la Mbeya lageuka kero kwa kusababisha mitaa kukithiri kwa uchafu, wananchi walalamika huku uongozi ukikiri kulemewa #MWANANCHI #JAN5
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Wilaya za Same, Mwanga na Siha zinakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na ukame uliosababishwa na uhaba wa mvua #MWANANCHI #JAN5
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Zaidi ya wakazi 3,000 wa kata ya Kiranyi, Arumeru waliojenga nyumba zao kwenye vyanzo vya maji wameamriwa kubomoa nyumba zao #MWANANCHI JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Waziri Ummy Mwalimu ameamuru uongozi wa Hospitali ya Geita kurejesha fedha za mzazi alizolipa kwa kununua dawa kinyume cha sheria #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Wizara ya Nishati na madini imetoa siku 14 kwa uongozi mgodi wa dhahabu Geita kuanza uzalishaji kabla haijafutiwa leseni #MWANANCHI #JAN5

Mwanafunzi wa darasa la saba Geita amekufa papo hapo huku wadogo zake wawili wakijeruhiwa kwa kupigwa na radi #MWANANCHI #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Bohari ya dawa imesema inahitaji zaidi ya bilioni 500 ili kukabiliana na upungufu wa dawa unaozikabili hospitali nyingi nchini #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Kaka ambaka mdogo wake wa kike mwenye miaka 15 na kumsababishia ujauzito, amkwamisha kujiunga kidato cha kwanza huko Bukoba #MWANANCHI #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Mbunge wa chama tawala Zimbabwe amefikishwa mahakamani baada ya kumtukana mke wa Rais wa nchini hiyo Grace Mugabe #MWANANCHI #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Serikali imepiga marufuku hospitali kupeleka wagonjwa hospitali binafsi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vinavyopatikana Muhimbili #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Bomoa bomoa yawakumbuka wachezaji wa Simba na Yanga, nyumba zadaiwa kujengwa katika maeneo hatarishi, ipo pia nyumba ya Bambo #NIPASHE #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Rais KAGAME wa Rwanda amesema kuna vitu vingi vya kukatisha tamaa katika dunia hii ambavyo Marekani ingepaswa kuvijali zaidi #NIPASHE #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
60% ya wagonjwa wanaotibiwa hospitali na Zahanati za umma nchini, wanahudumiwa na wauguzi wasio na ujuzi wa kutosha #NIPASHE #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Wananchi wa Kilosa wameiomba Serikali kuwapokonya ranchi za Taifa wamiliki waliokabidhiwa na kushindwa kuziendeleza #NIPASHE #JAN6
— millard ayo (@millardayo) January 6, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE