Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Hoteli zatikisika, wamilika wazigeuza kuwa hosteli, vyuo na nyingine zapigwa kufuli’
#MTANZANIA Hoteli zageuzwa hosteli, wamiliki wapunguza wafanyakazi ili kukabiliana na athari za ukosefu wa mapato pic.twitter.com/g67zoMZfLX
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
Gazeti hilo limekuja ripoti hii ya hoteli nchini kutisika ambapo limeripoti kuwa uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano kubana matumizi kwa kuzuia wizara, taasisi na mashirika ya umma kufanya mikutano kwenye hoteli pamoja na kodi sasa machungu yameanza kuuma kwa wamiliki wa biashara hiyo.
Kutokana na hatua hiyo, hoteli maarufu zilizopo Dar es salaam pamoja na mikoa mingine zimelazimika kufungwa na huku nyingine zikibadilishwa na kuwa hosteli kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kati.
Mbali na hilo pia baadhi ya wamiliki wa hoteli hizo wamelazimika kupunguza wafanyakazi kama njia ya kukabiliana na athari za ukosefu wa mapato.
Baada ya kuapishwa na kuingia madarakani Novemba 5 mwaka jana Rais Magufuli alitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi yasiyo ya lazima ikiwamo kuwataka watendaji wa mashirika ya umma kutofanya mikutano katika kumbi za mahoteli na ikiwezekana wafanyie chini ya miti.
Uchunguzi uliofanywa na mtanzania kwa wiki mbili sasa umegundua kufungwa kwa hoteli maarufu jijini Dar es salaam na nyingine mkoani Pwani, hoteli ambazo zimefungwa kutokana na sekeseke hilo ni Land mark hotel iliypo ubungo Dar es ambayo kuanzia September mosi itaanza kutoa huduma za hosteli.
Kwa upande wa hoteli ya Jb Belmont zilizopo katika majengo ya Benjamini Mkapa na Golden Jubilee jijini Dar es salaam nazo zimefungwa huku walinzi wakibaki kuzunguka katika maeneo hayo kulinda mali.
Unaweza kuzipitia habari zingine kubwa kwenye magazeti ya leo
#RaiaTANZANIA Halmashauri ya mji wa Njombe kinara wa usafi Tanzania, Mpanda yashika nafasi ya pili, kondoa ya tatu pic.twitter.com/NZ6ACXLdVM
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#NIPASHE JPM amwahidi kazi kwa utani Meya UKAWA, Mwita kama atafukuzwa kutokana na kusifia kazi ya Serikali yake pic.twitter.com/UwBFO3bXg7
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#NIPASHE JPM akaripia JKT, magereza kwa kutengeneza idadi ndogo ya madawati kutokana na bil 4 zilizotolewa na bunge pic.twitter.com/5YPh89o4k6
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#NIPASHE Sumaye akubali ombi la viongozi wa CHADEMA Pwani waliomchukulia fomu ya kuwania uenyekiti wa kanda hiyo pic.twitter.com/5S3l6rjvDg
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#NIPASHE Uhaba wa madawati shule ya msingi Sengerema umesababisha baadhi ya wanafunzi wa awali kukalia mikeka pic.twitter.com/smoKM3hvHd
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#NIPASHE Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 kutokana na kutochapishwa kwa miaka mitatu mfululizo pic.twitter.com/ulYmNLbB3y
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#NIPASHE TPA kuweka mfumo maalum ambao utawezesha muda wa ukaguzi wa malori bandarini kupungua na kuwa sekunde moja pic.twitter.com/hS40sRE9s1
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MWANANCHI Mwanamke aliyekatwa matiti ajifungua mtoto wa kike Moshi huku changamoto ikiwa ni jinsi ya kumnyonyesha pic.twitter.com/Xj9tQQkz68
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MWANANCHI JK asema wakati Tanzania ikitarajia kuwa nchi ya viwanda inatakiwa kuacha kupuuza mabadiliko ya tabianchi pic.twitter.com/vqkw9MroiX
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MWANANCHI Baadhi ya maofisa JNIA waliokuwa kwenye mashine za ukaguzi JPM alipofanya ziara waondolewa kitengo hicho pic.twitter.com/VNWuOna2sq
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MWANANCHI DC Gondwe azitaka taasisi za umma zilizolimbikiza ankara za maji kulipa ili kufanikisha upatikanaji wake pic.twitter.com/omHqvBl9V7

#MWANANCHI TAKUKURU K'njaro imeokoa mil 290.8 zilizoibwa kwa njia ya kifisadi kipindi cha mwaka mmoja kilichopita pic.twitter.com/HFMJpIwUaF
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MWANANCHI Tetemeko la ardhi Dodoma ladumu kwa sekunde 30, lina ukubwa unaokaribiana na lililotokea mwaka 2007 pic.twitter.com/ar9YwAYk0D
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MWANANCHI Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya usafiri wa anga, Hamza Johari amesema wameingia mikataba 60, inayotumika ni 20 pic.twitter.com/yBJGRbihpz
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MTANZANIA JPM awakutanisha Naibu Spika na baadhi ya wabunge wa UKAWA ktk ugawaji wa madawati 60,000 kwa majimbo 155 pic.twitter.com/iMkDI9v7EC
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#MTANZANIA Wanaokula Sokwe waonywa kwa kuwa wanabeba virusi vya magonjwa yanayoweza kusababisha kifo kwa binadamu pic.twitter.com/RV049Yqimf
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#HabariLEO Waziri Tizeba amewasimamisha kazi wakurugenzi watano idara tofauti baada ya kuonesha udhaifu ktk utendaji pic.twitter.com/II3zVNiNi2
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
#HabariLEO Mwalimu shule ya serikali Morogoro agundulika kuajiriwa mara mbili ikiwamo shule nyingine binafsi pic.twitter.com/2bg6dct8SZ
— millardayo (@millardayo) July 14, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 14 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI