Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Twitter basi taarifa hii kutoka kwao itakuwa inakuhusu moja kwa moja mtu wangu.
Tarehe 12 August kampuni ya Twitter imetangaza mabadiliko ya matumizi ya mtandao huo…kwanzia sasa kutuma message za private kwa njia ya Twitter imeboreshwa kufikia matumizi ya maneno 10,000 na sio maneno 140 kama ilivyokuwa hapo mwanzo.
Taarifa hii ilitolewa na Sachin Agarwal amabye ni product manager wa mifumo ya message ya Twitter na sababu ya wao kufanya mabadiliko haya yametokana na maombi mengi kutoka kwa watumiaji tofauti duniani wa huduma hiyo.
>>>“wateja wetu wengi wanaotumia private messages za Twitter wamekuwa wakiomba tuwaongezee maneno ili waweze kusema kile walichokusudia bila kuwaza kikomo cha kufikia maneno 140…lakini hii haimanishi kuwa tweets za kawaida zitaongezeka maneno pia No. Tweets za kawaida zitabaki na kikomo kilekile cha herufi 140 tu”.<<< Sachin Agarwal.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos