Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti August 28 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Mganga wa kienyeji Mkuranga amemtabiria mgombea Urais wa upinzani iwapo ataendelea kutumia fedha kurubuni wananchi atapoteza maisha #RaiaTZ
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Dk.SLAA huenda akaibuka kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama chake uliopangwa kufanyika kesho viwanja vya Jangwani #RaiaTZ AUGUST — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mwanamke omba omba na mwanaye wauawa kwa risasi Rombo na watu wanaodhaniwa ni majambazi #RaiaTZ #AUGUST28 http://t.co/Rxo383GzC5
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mama LOWASSA amewataka wenye maswali kuhusu mumewe aulizwe yeye, mumewe asema hayo ni zaidi ya mapenzi anayoonyeshwa na mke wake #RaiaTZ — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Familia ya watu tisa yateketea kwa moto Dar ikiwa imekumbatiana chumbani,mashuhuda walishindwa kuokoa baada ya moto kuzidi #MWANANCHI AUGUST
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Baada ya kushambulia Dar na Morogoro, ugonjwa wa kipindupindu waingia Pwani na tayari watu 9 wameonekana kuwa na dalili #MWANANCHI #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
LOWASSA amesema mabadiliko katika nchi hii ni jambo la lazima na linahitaji nguvu ya wanawake ili kulifanikisha #MWANANCHI #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Hatimaye CHADEMA wameruhusiwa kutumia viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kuzindua kampeni za mgombea wake wa Urais #MWANANCHI #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
NEC imekabidhi Polisi orodha ya majina 52,000 ya waliojiandikisha zaidi ya mara moja wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Vyama vya siasa vimetakiwa kutangaza sera zao na mafunzo ya kupiga kura kwa wanachama kabla ya Oktoba badala ya kupigana vijembe #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mkazi wa Morogoro anashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa amevaa sare za JWTZ, alikua akisubiri usafiri kutoka MORO kwenda Dar #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Idara ya Uhamiaji Mbeya imemkamata raia wa Zambia kwa kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura na kuishi nchini bila kibali #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Utafiti uliofanyika Uingereza unaonyesha kuwa unywaji wa pombe unasaidia kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo #MWANANCHI #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mwanamke ajifungua mtoto wa kiume akiwa kwenye usingizi wa kifo Carlifonia, alifanyiwa upasuaji wa ubongo na kushindwa kuzinduka #MWANANCHI — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Moto wateketeza malori mawili ya mafuta Mwanza, chanzo ni umeme wa jenereta uliokuwa ukitumika wakati wa kuhamisha mafuta #MWANANCHI AUGUST
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Moto wateketeza malori mawili ya mafuta Mwanza, chanzo ni umeme wa jenereta uliokuwa ukitumika wakati wa kuhamisha mafuta #MWANANCHI AUGUST — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MESSI atwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka Ulaya akiwabwaga wenzake RONALDO na Luis SUAREZ #MWANANCHI #AUGUST28 http://t.co/Rxo383GzC5
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Taifa Stars iliyopo kambini Uturuki ikijiandaa na michuano ya AFCON leo inataraji kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Libya #MWANANCHI AUGUST — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Aliyekuwa mbunge wa Longodo Lekule LAIZER amemweleza mgombea mwenza wa CCM kwamba kitendo cha LOWASSA kuhama kimewagawa wananchi #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Chama cha wanasheria nchini TLS kimelaani kitendo cha mwanachama wake Lawrance MASHA kunyimwa dhamana mahakamani #MTANZANIA #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Chama cha wanasheria nchini TLS kimelaani kitendo cha mwanachama wake Lawrance MASHA kunyimwa dhamana mahakamani #MTANZANIA #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mama LOWASSA amesema anashindwa kuelewa ni kwa nini watu wanatunga uongo kuhusu mume wake, yeye ni mtu pekee anayemfahamu mumewe #MTANZANIA — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MAGUFULI amesema Taifa linahitaji mabadiliko ya kuongoza nchi na siyo kwa kubadili chama kilichopo madarakani #MTANZANIA #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mgao wa umeme umeanza tena kwa siku tano Dodoma baada ya kusimamishwa takribani kwa wiki mbili #MTANZANIA #AUGUST28 http://t.co/Rxo383GzC5 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Wananchi wa Kahama walioathirika na mvua ya mawe March3 wamevamia ofisi ya Kata ya Mwakata na kugawana mabati na vitu mbalimbali #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Chama cha Walimu Temeke kimesema wanaidai Serikali zaidi ya bilioni 1 kwa ajili ya nauli za likizo tangu Desemba 2013 #MTANZANIA #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Ujenzi wa daraja la Kigamboni wakamilika kwa 90%, mpaka kukamilika utakua umegharimu kiasi cha dola milioni 143 #MTANZANIA #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Serikali imeombwa kuhakikisha inapitia upya mfumo wa kumaliza kidato cha sita kwa kuwa uliopo una changamoto nyingi #MTANZANIA #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Katibu wa CCM Iringa amesema chama chake hakiwezi kushinda kwa nyimbo za TOT bali kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kushinda #MTANZANIA AUGUST
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
NEC imetoa siku 7 kwa wahamiaji waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kujisalimisha kabla ya kuchukuliwa hatua #NIPASHE #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Benki ya dunia imeipatia Tanzania mkopo wa bilioni 422 kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa huduma za afya kwa wajawazito na watoto #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Raia wa China amefikishwa mahakamani baada ya kukutwa na meno matatu ya Simba yenye thamani ya zaidi ya milioni 10 #NIPASHE #AUGUST 28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Idadi ya wakimbizi kutoka Burundi wanaoingia nchini wakikimbia machafuko yanayoendelea nchini mwao imefikia 87,500 #NIPASHE #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MBOWE amewataka wanachama wa chama hicho kesho wajitokeze siyo kwa maelfu bali kwa mamilioni katika uzinduzi wa kampeni zao #NIPASHE #AUGUST — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MBOWE amewataka wanachama wa chama hicho kesho wajitokeze siyo kwa maelfu bali kwa mamilioni katika uzinduzi wa kampeni zao #NIPASHE #AUGUST
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MAGUFULI amesema hana deni la kulipa kwa mtu yeyote akichaguliwa kuwaongoza Watanzania kwa kuwa hakutoa rushwa wakati wa utezi wake #NIPASHE — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Chama cha walimu Arusha kimeitaka Serikali iwalipe deni lao la bilioni 4.5 la kupandishwa madaraja, posho, na nyongeza ya mishahara #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Jukwaa la Wakirisho kanda ya Kaskazini limeiomba Serikali kupanga siku tofauti na J2 ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu #NIPASHE #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
NEC imetoa ufafanuzi kisheria kuhusu wagombea waliopitishwa katika majimbo yao bila kupingwa kwamba hawana haja ya kufanya kampeni #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Prof. BAREGU amesema kitendo cha CCM kufungua kampeni zake kwa kutumia lugha za kukera na kuzidisha muda wa kufunga ni ishara mbaya #NIPASHE — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MWIGULU amesema Dk.MAGUFULI hana rafiki hivyo wananchi wamchague ili aweze kutatua kero zao #NIPASHE #AUGUST28 http://t.co/Rxo383GzC5
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Tanzania imetajwa kuwa na waathirika wengi wa vipodozi vyenye viambata vya sumu vilivyopigwa marufuku na Serikali #NIPASHE #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Juma PINTO amechaguliwa M’kiti mpya wa kamati ya Miss Tanzania itakayosimamia shindano hilo kitaifa, atangaza kamati mpya #NIPASHE #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Ugonjwa wa Kipindupindu wazidi kushika kasi Dar na sasa idadi yafikia 405 kwa Wilaya mbili za K’ndoni na Ilala #JamboLEO #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MAGUFULI amewaomba Watanzania wote wakiwemo wa CHADEMA wampe kura zao ili iwe na nguvu ya kufanya kazi ya kuleta mabadiliko #JamboLEO AUGUST
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mama amwagiwa tindikali iliyomuunguza sehemu mbalimbali za mwili wake huko Tarime kutokana na ubishi wa kisiasa #JamboLEO #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mkazi wa Veta Dar agonga kichwa cha treni na kufariki hapo hapo, ilimpitia katikati na kutenganisha mwili wake #JamboLEO #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Serikali imetakiwa kubadili muda wa kuhitimu kidato cha sita ili wahitimu wapate muda wa kutosha kujiunga na JKT #JamboLEO #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Walimu Rufiji wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na kutolipwa mishahara yao kwa kipindi cha miezi minne sasa #TzDAIMA #AUGUST28
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
MENGI amesema Watanzania wasikubali nchi kugeuzwa kama ‘Supermarket’ kwa kuagiza kila kitu kutoka nje ya nchi #TzDAIMA #AUGUST28 — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Jukwaa la Wakristo Kaskazini limewataka viongozi wa kisiasa kutumia kauli za kistaarabu kunadi sera zao na kuepuka kuudhi Wananchi #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
Mama LOWASSA ameeleza kuhusu afya ya mume wake ambaye amekuwa akituhumiwa na wapinzani kwamba ni mgonjwa na kudai yuko fiti #TzDAIMA#AUGUST — millard ayo (@millardayo) August 28, 2015
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos