Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii ambayo hutumiwa na watu wengi katika kufikisha habari, taarifa, mawazo na maoni ambapo huwafikia watu wengi kwa wakati mmoja.
Kama ulipitwa na stori kubwa mchana wa leo May 2, 2017 kupitia twitter, basi hauna sababu ya kuwa na wasiwasi zaidi wa kuzikosa kwani nimekukusanyia hapa tweets sita zilizobeba stori kubwa mchana wa leo.
Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege 2 za Marekani za kuangusha mabomu zimefanya mazoezi kwenye anga la rasi ya Korea ili kuwapa taarifa. pic.twitter.com/A2A5pDdLua
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Jeshi la Marekani limesema mfumo wake wa THAAD unaotoa kinga dhidi ya makombora umeanza kufanya kazi ya ulinzi nchini Korea Kusini. #BBC pic.twitter.com/KHMXkK152k
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Mamlaka inayosimamia vyombo vya habari Sudan Kusini imezifunga ofisi za televisheni ya Al-Jazeera, imetakiwa kutofanya kazi zake nchini humo pic.twitter.com/2uujh1ahWc
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Kamati ya Bunge imemsamehe Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa kauli za kudharau Bunge April 4, 2017 pic.twitter.com/ZRdW7zgEjd
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Himid Mao wa AzamFC ameondoka alfajiri ya Mei 2 kwenda kufanya majaribio ya siku 15 katika timu Randers FC ya Ligi Kuu Denmark. pic.twitter.com/I0oJ1rAPAL
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
Bunge limeazimia kumsamehe Halima Mdee MB aliyepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bajeti baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha pic.twitter.com/KTMMBVoNJG
— millardayo (@millardayo) May 2, 2017
VIDEO: Binadamu mzee zaidi duniani anayepatikana Tanzania. Bonyeza play kutazama…