Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilieleza siku chache zilizopita kuwa wamemkamata mmiliki wa Kampuni ya Techno Net Scientific inayojihusisha na uingizaji na uuzaji wa kemikali zikiwemo kemikali bashirifu.
Kamshna wa Mamlaka hiyo alieleza kuwa mmiliki huyo alikamatwa kutokana na kukiuka sheria na taratibu na kughushi nyaraka…sasa leo May 19, 2017 Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele ametoa ufafanuzi kuhusu kampuni hiyo…
“Baada ya muda wa usajili kuisha Kampuni hii iliwasilisha maombi ya kuhuisha usajili wake ambapo kwa mujibu wa sheria ya kemikali ilipaswa kusitisha shughuli zake hadi pale cheti cha usajili kitakapopatikana.” – Samwel Manyele.
Operesheni ya Dawa za Kulevya inavyoendelea na hatua iliyofikia hadi sasa…