Club ya Yanga SC Jumanne ya January 15 2019 iliendeleza kucheza michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga, Yanga ilicheza nyumbani uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya Mwadui FC iliyopo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019.
Game hiyo ilimalizika kwa Yanga kuendeleza ubabe na kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ya Yanga yakipatikana kupitia kwa Ibrahim Ajib dakika ya 12, Amissi Tambwe dakika ya 39 na Feisal Salum dakika ya 58 wakati Mwadui FC wameambualia goli moja lililofungwa na Salim Aye dakika ya 82.
Baada ya mchezo huo waandishi wa habari walipata nafasi ya kuumuliza vizuri kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera, mshambuliaji wake raia wa Congo DRC Heritier Makambo ameenda wapi baada ya kuenea tetesi kuwa mchezaji huyo ameondoka kambini na kutimkia kusikojulikana.
“Tunatoka Mbeya City na ndege tunafika hapa Makambo anaenda nyumbani kwake, sasa wanasema Makambo ametoroka kambini wapi hatukuwa kambini, Makambo amefika hapa anaenda nyumbani kwake saa nane usiku anakamata ndege anaenda Congo, wanasema kazima Simu kazima simu wapi walio na namba ya simu ya Makambo ya Congo ni mimi na Kinondoki basi”>>> Mwinyi Zahera
Yanga sasa baada ya kupata ushindi huo inazidi kujikita kileleni na kuwafanya wafikishe point 53 wakikamilisha michezo yao ya mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara, wakati Azam FC wakiifuatia Yanga kwakuwa na point 40 ila wana viporo game mbili, wakati Simba SC wapo nafasi ya tatu wakiwa na point 33 wakiwa na viporo michezo mitano.