Leo January 15, 2018 Nchini Uganda Chama cha Mawakili kimefungua kesi kwenye Mahakama ya Kikatiba kupinga mabadiliko ya Katiba ambayo yameondoa kigezo cha umri wa ukomo kwenye kugombea Urais.
Siku za hivi karibuni Muswada huu ulipitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Yoweri Museveni kuwa Sheria ambayo imeondoa ukomo uliokuwepo awali wa miaka 75 kwa anayetaka kugombea.
Mawakili hao pia wanapinga suala la kuongezwa kwa kipindi cha uongozi wa Wabunge na viongozi wa serikali za mitaa kutoka miaka mitano hadi saba na kusema kuwa viongozi hawa watakuwa wanavunja kiapo cha kikatiba walichokula May, 2016 kwamba wataongoza kwa miaka mitano pekee.
TOP 3: Hadi kufikia June 2017 hawa ndio wachezaji matajiri Nigeria
Ajali ya HIACE iliyoua 11 Kagera, aligonga Malori mawili