Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa viongozi wa serikali duniani kuwa makini na jinsi wanavyotumia mitandao ya kijamii na wanayoyaandika au kuyapost.
Ameeleza hivyo akiwa anafanyiwa interview na kijana kutoka familia ya kifalme ya Uingereza Prince Harry ambapo alionya kwa ujumla matumizi mabaya ya mitandao ambayo yanapelekea kuongezeka kupotosha uelewa wa mambo ya msingi na kuongeza uvumi.
“Moja kati ya hatari kubwa sana za mtandao ni kwamba watu wanaweza kupata uhalisia tofauti kabisa, wanaweza kupewa taarifa ambazo zinawatengenezea upendeleo. Swali ni kwa njia gani tunaweza kuunganisha hii teknolojia ili kuruhusu sauti nyingi, mgawanyiko wa maoni bila kupelekea utengano kwenye jamii na kutafuta njia ya kupata muafaka. ” – Barack Obama
UPDATES: Kesi ya mke wa bilionea Msuya, Jalada lafika kwa DCI