Mariam Oberet anatuambia “Nikiwa naendesha gari nilisikia sauti inaniambia ruka kutoka kwenye gari niende nje, nami nikaruka, gari ikaenda kugonga mbuyu ikaharibika, ilikuwa December 4, 2011, kuna mtoto alikuja kunisaidia akanipa simu nikapiga kuomba msaada”.
Mariam >>> “Nilipoambiwa siwezi kutembea tena, kwakweli nilipokea taarifa hizi vibaya sana, niliumia sana nikawa napata hasira sitaki kuongea na mtu yoyote, namshukuru MUNGU alinitia nguvu, nikaona ni kitu cha kawaida, haikuwa rahisi”.
Mariam >>> “Nakumbuka Daktari aliniambia unaamini kwamba MUNGU yupo? nakumbuka nilimwambia sidhani kama MUNGU yupo sababu kama angekuwepo asingeruhusu hiki kitu kisitokee katika maisha yangu kwani mimi nimemkosea nini MUNGU”.