Serikali imetoa taarifa kuhusu tuhuma zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini na vya Kimataifa kuhusiana na ziara ya Rais wa China kuhusishwa na usafirishwaji wa meno ya Tembo kutoka Tanzania.
Waziri Benard Membe wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa amekanusha hii ishu kwenye bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Amesema “..Chanzo cha habari hizo ni taarifa ya taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini Marekani ijulikanayo kama Environmental Investigation Agency kama alivyosema Mheshimiwa Silinde.. Habari hiyo imekwenda mbali zaidi kwa kuituhumu nchi yetu na viongozi wake kwa kutojali wala kushughulikia tatizo la biashara haramu ya pembe za ndovu’
‘Napenda kuutarifu umma wa Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba madai yaliyotolewa na NGO hiyo ya Marekani ya kuihusisha ziara ya kihistoria ya Rais wa China kutembelea Tanzania kama nchi ya kwanza toka aingie madarakani na biashara ya pembe za ndovu hayana ukweli wowote” – Membe
Bonyeza hapa kusikiliza taarifa iliyoripotiwa na TBC 1
Unapenda stori kama hizi zisikupite? ungana na mtu wako Millard Ayo kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia moja kwa moja mtu wangu >>> Twitter Instagram Facebook