March 29 2016 bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Sasa leo March 31 2016 shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo >>> ‘kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa‘
‘Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya‘ – BBC SWAHILI.
Ulipitwa na hii? Matano ya kufahamu kuhusu daraja la Kigamboni kabla halijaanza kutumika siku 16 zijazo tazama hii video hapa chini
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE