Leo December 27, 2017 Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetoa siku 30 kwa viongozi wa Umma wakiwemo wapya wanaochaguliwa au kuteuliwa kuwasilisha hati rasmi ya Mali au Rasilimali zao na za wake na watoto wao kwa Kamishna wa Maadili.
Akitoa wito huo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela amesema kwa kuzingatia kifungu cha 9(1)(a) na (c) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma, kiongozi anapofika mwisho wa kutumikia wadhifa wake, anatakiwa kujaza fomu za tamko la Rasilimali na madeni na kuziwasilisha kwa Kamishna.
Jaji Nsekela amesema sekretarieti inawataka viongozi umma ambao hadi sasa bado hawajapata fomu watumie tovuti www.ethicssecretariat.go.tz ili kupata fomu hizo kwa urahisi na kuzijaza.
Pia amewataka viongozi hao kuziwasilisha fomu hizo katika ofisi za Sekretarieti ya maaadili ya viongozi wa umma, Kanda ya Dar es Salaam, Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Ziwa Mwanza na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
”Viongozi wanakumbushwa kuwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15(c) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma , kwa kiongozi kushindwa kutoa tamko bila sababu ya msingi,” – Jaji Nsekela
ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA DECEMBER 27 2017? UNAWEZA KUIANGALIA HAPA CHINI