Kama umebahatika kukatisha makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere pale eneo la mataa ya TAZARA utakuwa umekutana na bango linaloonesha dalili nzuri… ni dalili za ujio wa flyover, zile barabara ya juujuu kwa ajili ya kusaidia kuokoa foleni eneo lile.
Ilikuwa moja ya ahadi za Rais Magufuli alipokuwa akizindua Kampeni zake za Urais 2015, lakini kabla ya hapo wakati akiwa Waziri wa Ujenzi katikati ya mwezi October 2015 alisaini na Serikali ya Japan mkataba wa ujenzi wa flyover hiyo… unaweza kuicheki video yenye ramani kamili mzigo ukikamilika.
Kama hujaona mzigo wa Kigamboni juujuu ya bahari unaweza kucheki kwenye hii video yake mtu wangu… ni dalili nzuri, soon tunasahau kutegemea pantoni pekeake kuvuka.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.