Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata hatimae leo ameripotiwa kuhama rasmi kucheza Ligi Kuu England akiwa na club ya Chelsea na kurudi nyumbani kwao Hispania katika jiji alilozaliwa na Madrid na kujiunga na club ya Atletico Madrid ya Hispania.
Morata anajiunga na Atletico Madrid ambao ni wapinzani wakuu wa timu yake ya zamani ya Real Madrid kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu wa miezi 18, Morata ameondoka England baada ya kutokuwa katika mipango ya kocha wa Chelsea Maurizio Sarri aliyeamua kumleta Gonzalo Higuan.
Alvaro Morata alijiunga na Chelsea 2017 akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano akiweka rekodi ya uhamisho wa pound milioni 60 ila amejiunga na Atletico kwa mkopo wa miezi 18 wenye kipengele cha kumnunua jumla wakivutiwa nae kwa dau la pound milioni 48 katika mwaka mmoja na nusu aliyokaa Stamford Bridge Morata amecheza jumla ya game 72 na kufunga magoli 24.
Haji Manara katolea ufafanuzi tuhuma za kuita washabiki wapumbavu