Chama cha soka barani Ulaya UEFA leo Alhamisi ya February 28 2019 kimefikia maamuzi ya kumfungia nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos kwa kubaini kuwa alifanya kosa la makusudi ili aoneshwe kadi ya njano na akose mchezo wa marudiano.
Sergio Ramos leo amefungiwa mechi mbili kucheza za UEFA Champions League kufuatia kubainika kutenda kosa la makusudi katika game ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Ajax iliyomalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa 2-1.
Hivyo Ramos alilazimisha kutenda kosa la makusudi dakika ya 89 ili aoneshwe kadi ya njano, kwa ajili ya kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Ajax, kwa kawaida Ramos alikuwa na kadi mbili za njano hivyo kama angeepuka kupata kadi katika mchezo dhidi ya Ajax, kwa hulka yake angeweza kuja kupata kadi ya njano na kuzifanya zifikie tatu hatua ya robo fainali na kukos mchezo muhimu ambao ungeweza kuigharimu timu yake.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake