Ni wiki moja imepita tokea shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA litangaze tuzo za mchezaji bora wa FIFA wa mwaka na tuzo za goli bora la mwaka, tuzo za mwaka huu mastaa wa FC Barcelona Lionel Messi na staa wa Juventus Cristiano Ronaldo hawakuhudhuria.
Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah walikuwa miongoni mwa wachezaji ambao magoli yao yalikuwa yanawania tuzo ya goli bora la mwaka “Puskas Award” tuzo hiyo alifanikiwa kushinda MO Salah wa Liverpool kwani goli lake dhidi ya Everton ndio lilitajwa kuwa bora zaidi ya yote matatu.
Ushindi wa tuzo hiyo kwa MO Salah wengi waliona kuwa Ronaldo ndio anastahili kwani goli lake alilofunga akiwa Real Madrid dhidi ya Juventus ni goli bora, sasa leo Ronaldo amefunguka akizungumzia kukosa kwake tuzo ya ‘Puskas Award’ na kupewa MO Salah.
“MO Salah alistahili kushinda Puskas Award alifunga goli zuri, hebu tuwe wakweli na tusijidanganye goli langu lilikuwa bora, sijakasirishwa maisha yapo hivyo kuna wakati unashinda na kuna wakati unapoteza lakini kitu kinachonivutia kwangu ni kuwa katika kiwango cha juu kwa miaka yote 15 ya maisha yangu ya soka”>>>Cristiano Ronaldo
“Hongera pia kwa Modric kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa mujibu wa FIFA, tuzo ni tuzo tayari nimeshinda nyingi nacheza mpira kushinda na sio kushinda tuzo binafsi”>>> Cristiano Ronaldo
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga