Ni wazi sasa kocha msaidizi wa Simba SC Masoud Djuma nafasi yake ndani ya kikosi cha Simba imezidi kuwa ndogo, kufuatia taarifa za kuendelea kutoelewana na makocha wa wakuu wa club hiyo.
Masoud alikuwa akidaiwa kuwa ni chanzo cha mahusiano mabovu, kiasi cha kocha wa sasa Patrick Aussems kutotaka kuwa nae katika timu, zaidi ya mechi mbili Masoud Djuma alikuwa hayupo katika benchi la Simba kama kocha msaidizi zaidi ya kuonekana katika mchezo dhidi ya Yanga.
Baada ya headlines za hapa na pale kuwa anafutwa kazi, sasa kuna dalili kuwa si zaidi ya saa 24 club ya Simba itatangaza kumfuta kazi kocha huyo ambaye amekuwa akidaiwa kutokuwa na maelewano na makocha wote wakuu Simba SC kuaniza Joseph Omog, Pierre Lenchantre na sasa Patrick Aussems.
Kufuatia tetesi hizo kauli ya kaimu Rais wa Simba SC Salim Abdallah kupitia Azam TV inaashiria kuwa nafasi ya Masoud haipo tena Simba na sasa wanasubiria saa tu zitimie watangaze rasmi japokuwa hajataja watafikia maamuzi gani.
“Kama nilivyowahi kuongea awali yapo matatizo ambayo tulijaribu kuyatatua lakini tumeshindwa kuya-handle, maamuzi ni kwamba inafika hatua inabidi kuamua upande mmoja uathirike, kikubwa zaidi kesho tutakuwa tumetoa taarifa rasmi baada ya kukamilika kwa baadhi ya taratibu”>>>Salim Abdallah
“Kwa sababu mambo ya kimkataba na mambo mengine yana taratibu zake, kwa sasa tunajaribu kuona na kufanya kila linalowezekana hili jambo liweze kuisha vizuri ili heshima ya pande zote mbili iweze kuwepo”>>>> Salim Abdallah
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga