Pengine ulikuwa hujui jina BATE ni kifupisho cha Borisov Automobiles and Tractor Electronics, ndio! Nimetaja trekta, FC BATE inamilikiwa na kiwanda cha magari huko nchini Belarus. FC BATE wameshinda taji la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Belarus mara 13 mfululizo, hawa ndio watawakaribisha Arsenal katika uwanja wa Borisov Arena Alhamisi hii majira ya saa 20:55 Usiku.
Mchezo wa Arsenal ni moja kati ya michezo 16 itakayochezwa Usiku wa Alhamisi hii katika hatua ya 32 bora ya michuano ya UEFA Europa League, kwa upande Arsenal huenda wakaendelea kumkosa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Gabon Pierre Americk Aubameyang ambaye ni mgonjwa.
Hata hivyo Arsenal watajipa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo baada ya kushinda mchezo wa ugenini dhidi ya Huddersfield 2-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza. Itakumbukwa pia msimu uliopita Arsenal waliichapa BATE 4-2 ugenini na kisha 6-0 katika dimba la Emirates, hivyo wataingia uwanjani historia ikiwabeba.
Kwa upande wa Chelsea wao watahitaji kuwa na utimamu wa kimchezo baada ya kufungwa ugenini kwa Manchester City kwa magoli 6-0 Jumapili iliyopita. Chelsea pia watakuwa ugenini nchini Sweden kucheza dhidi ya Malmo FF. Malmo imewahi kushinda mara moja tu dhidi ya timu za Uingereza.
Michezo mingine itayakayochezwa Alhamisi Usiku Saa 2:55 ni SS Lazio vs Sevilla (Sports Premium), Krasnodar vs Leverkusen (Sports Arena) na ile ya Saa 5:00 Usiku ni Sporting CP vs Villarreal (Sports Focus), Celtic FC vs Valencia CF (Sports Arena), FC Zurich vs Napoli SSC (Sports Premium) na nyingine zote kupitia chaneli za michezo za StarTimes.
Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka