Mshambuliaji wa zamani wa club za Inter Milan, FC Barcelona na Man United Zlatan Ibrahimovic ambaye kwa sasa anakipiga katika club ya LA Galaxy ya Marekani, ameripotiwa kuzindua sanamu yake nchini kwao Sweden.
Sanamu ya Zlatan ambayo inatajwa kuwa bora zaidi ya ile ya Cristiano Ronaldo, imezinduliwa nchini kwake Sweden katika mji wa Malmo, hiyo ikiwa ni heshima kwa mchezaji huyo baada ya kufanya vizuri katika soka na kuitangaza vyema Sweden.
Zlatan amepewa heshima hiyo pia kutokana na kuwa mfungaji wa muda wote wa Sweden lakini pia kuwa mchezaji pekee wa Sweden aliyewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Sweden kwa zaidi ya mara nane mfululizo, sanamu hiyo imetengenezwa na Peter Linde raia wa Sweden na ina urefu wa futi 8.9.
VIDEO: Goli lililoipa Tanzania Ubingwa wa CECAFA U-20 dhidi ya Kenya