Baada ya Rais Magufuli kuwapa siku tano Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda kuondoa tofauti zao kabla hajachukua uamuzi wa kutengua uteuzi wao, Waziri Kigwangalla amesema tayari amekutana na Katibu Mkuu wake na wamemaliza tofauti zao.
“Kazi ya Urais ni ngumu sana, tulioteuliwa na Rais kumsaidia utendaji/usimamizi wa maeneo mbalimbali hatupaswi kumuongezea Rais frustrations nyingine zaidi, sisi kwenye Wizara yetu, baada ya kikao na Chief Secretary tulimaliza tofauti zilizokuwepo na sasa hali ni shwari”– WAZIRI KIGWANGALLA
BILA KUPEPESA MACHO MAGUFULI AMPA ONYO KALI KIGWANGALLA “NITAMTUMBUA ANAGOMBANA NA KATIBU WAKE”