Baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu kwamba Simba itaachana na kocha Goran Kopunovic kutokana na kushindwa kuafikiana kwenye maslahi, hatimaye klabu hiyo leo kupitia kurasa zake rasmi za Facebook na Twitter zimethibitisha ukweli wa tetesi hizo.
Goran ambaye alikuja Simba katikati mwa msimu ujao uliopita anadaiwa kuwa alitaka kulipwa fedha nyingi sana ili kuendelea kubaki Simba.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba kilifunguka kwa ripota wa millardayo.com kwamba Kopunovic alitaka kulipwa ada ya usajili ya $50,000 ambayo ni karibia na millioni 100 za kitanzania, huku akihitaji mshahara wa $14,000 ambayo ni sawa na millioni 28.
Simba ilishindwa kufikiana nae na hivyo ikamruhusu kuondoka mwishoni mwa wiki iliyopita.
Simba hivi sasa inatajwa kuanza kufanya mazungumzo na baadhi ya makocha akiwemo kocha wa kibelgiji Piet de Mol.