Naibu Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson jana August 14, 2017 alizindua mradi wa kuhamasisha jamii kupinga ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika kata ya Kitunda Manispaa ya Ilala.
Katika uzinduzi huo alieleza kuwa mradi huu pia unalenga kutoa hamasa kwa wanafunzi kumaliza masomo yao bila kujihusisha kwenye mahusiano ya kimapenzi hata kama wamevuka umri wa miaka 18 ili uwe msingi mzuri wa wao kujitengenezea maisha.
>>>”Ni vyema waelewe umuhimu wa kujiendeleza kielimu kwanza ili wapate shughuli ya kufanya kama ni kujiajiri au kuajiriwa, kwa sababu katika umri wa miaka 18 kijana huyu anakuwa bado hana uwezo wa kuendesha familia.” – Dr. Tulia.
“Kuna wanaume hawataki wake zao wafanye kazi” – Dr. Tulia Ackson…tazama kwenye video hii hapa chini kujua kila kitu!!!!