Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.
Akizungumza katika kikao kazi na Waziri wa Fedha na Mipango, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi CP Salum Rashid Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika kwamba tuhuma si za kweli wahusika watarejeshwa kazini.
Majaliwa alizitaja baadhi ya tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, Mwaka huu kupitia vocha 30 ya Milioni 251 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi hiyo maalum ni kazi gani na nani aliifanya hiyo kazi.
Amesema siku hiyo hiyo ya Machi 31 pia zililipwa Milioni 198.8 kwa madai kuwa ni posho ya Honoraria.
Majaliwa amesema Aprili 8 mwaka huu watumushi 27 wa Wizara hiyo walilipwa Milioni 44.5 zikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki nne. Pia Aprili 13 mwaka huu zililipwa Milioni 155.2 kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya ya kazi maalum ya wiki tatu.
Aidha, Aprili 30 mwaka huu zililipwa milioni 43.9 kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyo hiyo zililipwa sh miloni 14.4 kwa ajili ya siku ya wanawake. Fedha nyingine Milioni 43 zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa shilingi mikioni101.8.
Amesema kuwa, Mei 1 asubuhi mwaka huu zililipwa Milioni 184.1 na mchana zililipwa Milioni 264 zikiwa ni malipo ya kazi maalum. “Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho”
Aliongeza kuwa Mei 3 mwaka huu zililipwa Milioni 146.5 kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa Mpango Kazi wa Manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku. Tarehe hiyohiyo zililipwa Milioni 171.2 kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.
Majaliwa amesema Milioni 155 zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi. ” Yaani hii kazi ya ukaguzi ineliowa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongekea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukuwa huko mlikozihamishia.”
Majaliwa amewataka Watendaji wa Wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na alitahadharisha kuwa watakaoendekea kuchen na pesa za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza watendaji wengine wa wizara hiyo ambao wameendelea kufanya kazi kwa weledi “na nimesema hapa si wote wenzenu wachache wanatumia vibaya nafasi zao kutuchafua Wizara ya Fedha.