Kampuni ya Usafiri Mtandao Uber imetangaza kurudisha huduma zake rasmi hapa Nchini baada ya kusitisha huduma hizo tangu April mwaka jana kutokana na madai ya kanuni za Latra kutokuwa rafiki .
Uongozi wa kampuni hiyo umesema hayo Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari ambao umelenga kutoa taarifa hiyo ambapo amesema wamerejea baada ya kufanya mazungumzo na Latra na kufikia muafaka.