Club ya Azam FC imetangaza kuachana na Kocha wake Denis Lavagne Raia wa Ufaransa ikiwa ni siku 47 zimepita toka watangaze kumuajiri.
Taarifa ya Azam FC haijasema sababu ila za ndani zinadai kuwa Kocha hana mahusiano mazuri na wachezaji na hashauriki licha ya kukaa kwa muda mfupi.
Lavagne toka ajiunge na Azam FC ameiongoza katika michezo 7 mmoja wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe ulioisha sare 1-1 na ameshinda game 3 sare 1 na kupoteza game tatu #MillardAyoSPORTS