Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko katika uchaguzi wa rais na wabunge siku ya Jumatano baada ya kampeni za vurugu zilizogubukwa na shutuma za upinzani kuhusu wizi, ghasia za uchaguzi, na kukwama kwa vifaa ambavyo vinaweza kuwazuia wengi kupiga kura.
Kilicho hatarini siyo tu uhalali wa utawala unaofuata. Mizozo ya uchaguzi wa Congo mara nyingi huzua machafuko makali na madhara yake huwa makubwa.
Congo ni nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa shaba, na mzalishaji mkuu wa cobalt, sehemu ya betri inayohitajika kwa mabadiliko ya Nishati mbadala iliyo safi.
Uchelewesho uliripotiwa katika miji kadhaa ya mashariki mwa Congo iliyo na matatizo ya kupambana na waasi na katika mji mkuu Kinshasa, vifaa vya kupigia kura havijafika katika vituo vya kupigia kura na orodha za wapiga kura haijachapishwa
Ni vurugu kabisa, alisema mgombea urais Martin Fayulu, mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2018 ambao ulikuwa na utatanishi.
Fayulu alisema kuwa wakati upigaji kura ulikwenda vizuri katika wilaya ya Gombe katika mji mkuu ambako alipiga kura na haikuwa hivyo katika maeneo mengine ya nchi.