Rais wa Comoro anayemaliza muda wake , Azali Assoumani, 65, ametangazwa mshindi siku ya Jumanne katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais uliyofanyika siku ya Jumapili katika visiwa vya Bahari ya Hindi, huku upinzani ukikashifu udanganyifu katika uchaguzi huo.
Mwanajeshi huyo wa zamani, ambaye atarejea kwa muhula wa tatu mfululizo, amepata 62.97% ya kura zilizopigwa, ametangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Idrissa Said Ben Ahmada Jumanne jioni.
Wagombea wa upinzani wamelalamika kwamba kulikuwa na “udanganyifu” na “ujazaji masanduku karatasi za kura zilizokwishapigwa.”
“Kama ilivyokuwa mwaka 2019, tunashuhudia udanganyifu (mwingine) kwenye uchaguzi ukifanywa na Azali Assoumani akishirikiana na jeshi,” amesema mmoja ya wagombea wa kiti cha urais, Mouigni Baraka Said Soilihi, alipozungumza na waandishi habari.
Rais Assoumani ambaye anatawala visiwa vya Comoro tangu mwaka 2016 alirefusha muhula wake madarakani kupitia mabadiliko tata ya katiba.
Mabadiliko ya katiba ya baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2019 yaliyoondoa sharti la nafasi ya urais kuwa ya kupokezana miongoni mwa visiwa vitatu vikubwa vinavyounda Jamhuri ya Comoro.