Mlinzi wa kimataifa wa Kenya, Jockins Atudo, ambaye amerejea kwao kujiunga na Tusker FC baada ya kucheza kwa msimu mmoja katika klabu ya Azam FC, amezungumzia suala la uchawi katika mchezo wa soka nchini Tanzania.
Akizungumza baada ya kutambulishwa jana katika uwanja wa mazoezi wa Tusker, Atudo alisema ingawa kumekuwepo na tetesi za uchawi katika soka hasa Bongo, alisema kwamba hajawahi kushuhudia vitendo vya imani ya kishirikina katika muda wote aliowahi kukaa nchini Tanzania kwenye klabu ya Azam FC.
“Maneno maneno yapo lakini sie tulicheza vizuri bila kujihusisha na uchawi wala waganga. Sikuwahi kushuhudia hata kitendo kimoja kinachohusiana na imani za kishirikina,” alisema.