Uchunguzi kuhusu sababu za ajali ya Titan chini ya maji umeanzishwa na Walinzi wa Pwani ya Marekani.
Mpelelezi mkuu Cpt Jason Neubauer alisema kipaumbele chake ni kupata mabaki ya nyambizi ndogo, tahadhari zitachukuliwa iwapo mabaki ya binadamu yatapatikana.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari, pia alisema uchunguzi huo utawezesha kupendekeza mashtaka ya kiraia au ya jinai.
Kikosi hicho cha walinzi wa pwani wa Marekani kitashirikiana na mashirika mengine ya kimataifa, ikiwemo bodi ya usalama wa usafiri ya Canada na tawi la uchunguzi wa ajali za baharini la Uingereza, miongoni mwa mengine kuchunguza ajali hiyo iliyotokea Juni 18 na iliyofuatiliwa duniani kote.
Jana mkuu wa shughuli ya uchunguzi wa kikosi cha walinzi wa pwani cha Marekani, Kapteni Jason Neubauer, alisema operesheni ya kuitowa nyambizi inaendelea na tayari wameshatambua ilikotokea ajali, ingawa hakutowa muda wa kumalizika uchunguzi