Uchunguzi wa mahakama umefunguliwa Jumanne nchini Kongo baada ya vifo vya ghafla vya vijana wasiopungua 37 katika mkanyagano uliotokea siku moja kabla ya operesheni ya kusajili wanajeshi katika mji mkuu Brazzaville.
“Idadi ya muda iliyotangazwa na idara ya huduma za dharura inabaini kwamba watu 37 walifariki na wengi kujeruhiwa,” inabaini taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kitengo maalumu kilichoanzishwa na Waziri Mkuu Anatole Collinet Makosso, akimaanisha “janga” kwa Congo.
Picha nyingi, zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha makumi ya miili ya watu waliofariki iliyohifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha manispa ya mji wa Brazzaville, pamoja na watu waliojeruhiwa waliolazwa katika kituo cha hospitali ya chuo kikuu (CHU) cha Brazzaville na hospitali ya kijeshi. Jeshi la Kongo lilitangaza wiki iliyopita kuajiri vijana 1,500 wenye umri wa miaka 18 hadi 25.
Jumatatu usiku, vijana waliokuwa wakijiandikisha waliiingia kwa nguvu na kuvunja lango la uwanja wa soka Michel d’Ornano, ambapo zozi hilo linafanyika, katikati mwa jiji la Brazzaville. Mkanyagano ulitokea, ambapo watu wengi walianguka na kukanyagwa, wakaazi wamesema. Baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya, kulingana na shuhuda kutoka familia za waathiriwa.