Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Mabasi ya haraka kuanza kutumia gesi’
#HabariLEO Imeelezwa kuwa awamu ya pili ya mabasi ya haraka yatatumia gesi asilia badala ya mafuta pic.twitter.com/w8VzMn7g9X
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
Gazeti la Habari Leo limeripoti kuwa` msimamizi wa usambazaji gesi katika shirika la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama.
Kupitia gazeti hilo Naleja amesema matumizi ya nishati hiyo yataanza katika awamu ya pili ambapo mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.
Akizungumza katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongezeka idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.
>>>’‘Uendeshaji wa gesi utakua nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi itatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu”
Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya July 04 2016
#NIPASHE Abiria 10 kati ya 30 wahofiwa kufa maji Songea vijijini, mkoani Ruvuma baada ya boti kuzama kwenye maji pic.twitter.com/NoSQ19w3Ni
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MWANANCHI Kauli ya Kamishna TRA dhidi ya benki zinazotoza VAT kwa wateja wao imezidi kupingwa na wasomi, wachumi pic.twitter.com/uolSKSF3FU
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MWANANCHI Kundi la watu wasiojulikana wavamia ofisi za Ahsante Tours Moshi, waua walinzi wawili na kupora mil 65 pic.twitter.com/R9roXWvrVs
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MWANANCHI Mjamzito mmoja Shy ajifungulia kwenye korido la kituo cha afya cha Lyabukande baada ya kukosa huduma pic.twitter.com/bAWYHYkeVh
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MWANANCHI Majaji 14 kuanza kozi maalumu ya siku tano kujifunza sheria mpya za kuendesha mashauri ya wahujumu uchumi pic.twitter.com/IjKZltVNlW
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MWANANCHI Wananchi walalamikia kuzuiliwa mlangoni sabasaba iwapo hawana risiti ilhali baadhi ya wahusika hawatoi pic.twitter.com/UbBJyqGuPQ
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#JamboLEO TANESCO yadaiwa kumpa taarifa za uongo Waziri Muhongo kuhusu malipo ya fidia kwa wakazi 500 wa chamazi pic.twitter.com/G0ZRa9zhls
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#HabariLEO Jaji Mkuu, Chande amesema kesi za mafisadi kutozidi miezi tisa na kwamba mahakama itaanza na majaji 14 pic.twitter.com/wVRKGBcWUy
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#HabariLEO Panya wa SUA wanaotegua mabomu, kubaini kifua kikuu soko lake laongezeka baada ya nchi nyingi kuwahitaji pic.twitter.com/ofyqE7OAe5
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#HabariLEO Utafiti UDSM wabaini 70%-90% ya wanawake nchini wameshambuliwa na aina mbalimbali za vijidudu vya fangasi pic.twitter.com/cpQt4wsnwg
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MTANZANIA TAKUKURU imewatia mbaroni wamiliki wa kampuni zinazodaiwa kukwepa kodi kwa kutengeneza stakabadhi feki pic.twitter.com/Z9AXx5cNSj
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MTANZANIA Waingereza ndio watu wenye ubinafsi zaidi duniani, ndiyo jamii inayokazia zaidi faida za kibinafsi pic.twitter.com/aXBCtjTGP1
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MTANZANIA Wauguzi Mirembe ambayo hutibu vichaa wamesema wamekuwa wakipigwa na wagonjwa wakati wakiwahudumia pic.twitter.com/mh0SD1ZepH
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
#MTANZANIA Mwili wa mbunge wa zamani wa kilindi, Beatrice Shelukindo 'CCM' unatarajiwa kuzikwa alhamisi wiki hii pic.twitter.com/6e5W30XCBq
— millardayo (@millardayo) July 4, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 4 2016 AYO TV? UNAWEZA KUITIZAMA VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE