Baada ya May 28 2016 Serikali kuwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu Dodoma. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mgomo wa walimu uliokuwa umedumu kwa takribani wiki 3.
Taarifa iliyotolewa leo na waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Joyce Ndalichako amesema kwamba baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, Serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao.
Baada ya uchambuzi huo leo July 19 2016 Serikali imetangaza kuwa wanafunzi 382 (mwaka wa kwanza 134 na wa pili 248) ambao wana ufaulu wa daraja la kwanza na la pili ambao pia wamefaulu masomo ya sayansi ndiyo pekee watakaorudishwa katika chuo kikuu cha Dodoma na wengine watasambazwa kwenye vyuo vya ualimu mbalimbali ili wakamalizie mafunzo yao.
ULIKOSA HII SABABU YA WANAFUNZI VYUO VIKUU KUTOPATA FEDHA ZA ‘FIELD’ MPAKA SASA ? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI