Ujuzi wa mawasiliano na maadili ya kazi zimeonekana kuwa changamoto kubwa kwa wahitimu wanaoajiriwa kwenye makampuni.
Hayo yalibainishwa na wakurugenzi watendaji taasisi ya fedha wa makampuni mbalimbali ikiwemo taasisi za fedha, kilimo cha bustani, utengenezaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Viwanda mandhari ikiwa mpango wa mazungumzo ya ushirikiano wa mikakati iliyoandaliwa na udsm kwa kushirikiana na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF).
“Hizi ni changamoto ambazo ni endelevu hivyo tunawashauri chuo Cha UDISM na vyuo vingine waone ni namna gani wanaweza kuongeza kwenye mitaala ya chuo kuwezesha wanafunzi wakihitimu waweze kuwa wenyewe uwezo kuajiriwa na kujiari,” hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji Multchoice,” Jacqueline Woiso.
Akizungumzia suala la maadili ya wafanyakazi alisema vijana wengi wanaoanza kazi wanataka wapate pesa nyingi kwa haraka ya kuweza kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja wakati ndio ameanza kazi. Mawazo yake yanaposhindwa ndio wanaanza kudokoa,”.
Alitaja changamoto nyingine kwa wahitimu hao ni uwezo wa kutoa huduma kwa wateja.
” Wahitimu wengi wakiajiriwa bado tunapata shida kumuelimisha kuwa mteja ni mfalme ambaye anapaswa kuhudumiwa vizuri,” alisema.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Jamal Ali ambaye alikuwa Mgeni Rasmi amesema kupitia mradi wa HEET serikali imefanya jitihada ya kutafuta fedha kwa lengo ni kufanya kuboresha mitaala itakayofundisha vijana ambao itaendana na mahitaji ya soko.
“Kupitia mradi huu wa HEET tunataka kuona taasisi zetu zikishirikiana kwa karibu zaidi na wadau wake amabo ni sector binafsi, sector za waajiri na hata kujenga uwezo wa vijana wetu kuweza kujiajiri,”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Raphael Maganga alisema ushirikiano kati ya wanachuo wa Serikali na sekta binafsi umekuja wakati mwafaka.
Alisema sekta binafsi ina nafasi muhimu kwani hainufaiki tu na wafanyakazi wenye ujuzi bali pia ina utaalam wa kitaalamu na maarifa juu ya ujuzi unaohitajika na soko la ajira.
“Sisi kama sekta ya kibinafsi lazima tushiriki kikamilifu katika wigo mzima wa mafunzo ya ujuzi programu kutoka kwa usanifu na utoaji hadi kuwezesha kazi za uga wa saruji na mafunzo,” alisema Bw Maganga.
Alisema kwa kufanya hivyo sekta binafsi inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mfumo mpana zaidi na unaounganishwa.
Bw Magana alisema jukumu muhimu la sekta ya kibinafsi ni pamoja na ushiriki katika Programu za Mafunzo ya Ujuzi ambazo zinahakikisha sekta binafsi kuwa na programu ya mafunzo ya ugani, ushirikishwaji na utofauti, Mbinu inayolenga Soko na Kujitolea kwa Waajiri.
Mengine ni Mafunzo yenye mwelekeo wa Matokeo, kujitolea kwa Mkurugenzi Mtendaji na programu za ushauri na Utendaji pamoja na kuweka utaratibu wazi wa kutambua waajiri watarajiwa katika kulisha taarifa kwenye mfumo wa taarifa wa soko la ajira la taifa.
Kwa upande Wake Makamu Mkuu wa UDSM , Profesa William Anangisye alisema lengo la mkutano huo ni kufanya mazungumzo ya kimkakati kati ya chuo hicho na wadau kutoka sekta binafsi na kujifunza kutoka kwao.
Alisema wanataka kuona utekelezaji wa mradi wa HEET unakuwa na mafanikio katika mageuzi ya elimu.
” Huu ni mkakati tumekutana na wakuu wa taasisi wao watasaidia kutueleza changamoto wanazokutana nazo kupitia wahitimu wetu lakini pia ni lazima wahitimu wawe na uwezo na mtazamo wa kusaidia nchi kuleta mageuzi,” alisema.