Chama cha soka Ulaya (UEFA) kimepinga madai kuwa kuna pendekezo kutoka shirika la afya duniani (WHO) kuwa linawataka kuwa waahirishe michuano yote ya kimataifa hadi mwisho wa mwaka 2021 sababu ya corona.
UEFA inaamini hiyo sio sahihi kwa maana hiyo mpira utakuwa hauchezeki, awali UEFA ilikubali kuahirisha michuano ya Euro 2020 baada ya kushauriana na WHO.
Msemaji wa UEFA alinukuliwa akisema “Hii sio sawa WHO hawajawahi kupendekeza hivyo kuwa mpira hautachezwa hadi mwisho wa mwaka 2021”
WHO ndio walioishauri kamati ya kimataifa ya Olympic (IOC) kuahirisha michuano ya Olympic iliyokuwa ichezwe Tokyo kwa mwaka mmoja na walishauri pia kuahirishwa kwa Euro 2020 kwa mwaka mmoja hadi 2021 sababu ya corona.