Muungano wa Mashirikisho ya Soka ya Ulaya (UEFA) umekosolewa vikali na watumiaji wa mitandao ya kijamii baada ya kudai kuwa “haina nia” ya kuiondoa Israel nje ya michuano ya Ubingwa wa Uropa kutokana na vita inayoendelea ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
Katibu Mkuu wa bodi ya UEFA, Theodore Theodoridis, alikataa kuipiga marufuku Israel baada ya kundi la Vyama vya Soka vya Mashariki ya Kati kutaka utawala huo na kutaka uondolewe kwenye mashindano ya dunia kutokana na vita vinavyoendelea Gaza.
Hii ni katika hali ambayo, hapo awali Aleksander Ceferin, Rais wa UEFA aliiambia Telegraph Sports kuwa, kushiriki Israel na Ukraine kwenye mechi za EURO 2024 kunaweza kuwa tishio la usalama kwa mashindano hayo ya kieneo yanayotazamiwa kufanyika katika msimu ujao wa joto kali nchini Ujerumani.